Wanarukwa waaswa kuilinda amani kuelekea uchaguzi 2020

  Masama Blog      Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka wananchi wa mkoa wa Rukwa kuhakikisha wanawaepuka wanasiasa wenye lengo la kuvuruga amani na mshikamano wa wanarukwa, kusababisha mifarakano baina ya wananchi na hatimae kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo katika mkoa.

Amesema kuwa umuhimu wa kuilinda amani unatokana na upekee wa mwaka 2020 kwakuwa ndio mwaka wa uchaguzi mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais, na kutahadharisha kuwa katika kuelekea kwenye uchaguzi huo kutakuwa na harakati kadhaa za kisiasa, na kuwataka wanarukwa kuwaepuka wanansiasa wasioitakia mema nchi yetu.

Mh. Wangabo ameyasema hayo alipokuwa akitoa salamu zake za mwaka mpya katika ibada ya kuukaribisha mwaka 2020 iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kristu Mfalme, mjini Sumbawanga.

“Tuwaepuke wanasiasa wa namna hiyo ili tudumishe umoja wetu, amani yetu na mshikamano wetu, Tusikubali kuyumbishwa na wanasiasa katika kipindi cha mwaka huu, ni mwaka wa uchaguzi kila mtu anataka kupitia migongo ya wananchi ya wanarukwa ili kutimiza matakwa yake,” Alisema.

Aidha, aliwataka wananchi hao kuzingatia kuwa miaka yote wanarukwa wamekuwa wamoja na hawajawahi kuyumbishwa na pia maisha baada ya uchaguzi na hivyo kutoshawishiwa kwa urahisi na watu wachache wanaotaka kutekeleza matakwa yao yasiyoitakia mema amani iliyopo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/39uzCr4
via
logoblog

Thanks for reading Wanarukwa waaswa kuilinda amani kuelekea uchaguzi 2020

Previous
« Prev Post