Ticker

10/recent/ticker-posts

Wamshukuru Rais Dkt Magufuli kuongeza muda kujiandikisha Nida


Woinde Shizza, Arusha

Wananchi mkoa Wa Arusha wamemshukuru Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kitendo cha kuwaongezea muda Wa kusajili laini zao za simu kwa alamaza vidole,kwani ni asilimia kubwa ya wananchi walikuwa bado hawajasajiliwa laini zao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa kujiandikisha na kusajili namba zao za Nida linaloendelea katika viwanja vya kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid walisema kuwa asilimia kubwa ya wananchi hawajasajili laini zao kwa alama za vidole kutokana na kutokuwa na namba za Nida .

"Foleni hii kubwa sio kusajili kwa alama za vidole hapana, foleni hii imetokana na wananchi wengi hatuna namba za Nida ,kama Mimi nimejiandikisha tangu mwaka Jana zoezi lilivyoanza lakini hadi Leo sijapata namba wala kitambulisho ninekuja Mara kibao Mara niambiwe sionekani kwenye taarifa zao za Nida ,muda mwingine unakuta picha lakini huoni namba " alisema Steven John

Walitumia muda huo kuomba Nida kuongeza wafanyakazi pamoja na vitendea Kazi ili zoezi liweze kwenda kwa haraka huku wakiwasisitiza kufungua mapema vituo vyao vya kuangalia namba za vitambulisho pamoja na kujisajili .

"Leo wengine tumekuja SAA kumi na moja usiku ,wengine Saa moja tumekaa hapa Nida wamekuja kufungua SAA tatu jamani kweli tunaomba wawahi basi kufungua ili watu waweze kufungua haraka na kiurahisi maana watu ni wengi sana na ikiwezekana muda Wa Kazi uongezwe tunaomba ili tupate huduma"Gloria Oktavina

Akizungumza na Wananchi hao katika zoezi hilo Mkuu Wa mkoa Wa Arusha Mrisho Gambo aliwapongeza wananchi kwa namna ambavyo wamejitokeza kujiandikisha na kusajili namba zao kwa uvumilivu , alisema kuwa serikali imejipanga vyema kuhakikisha zoezi hili linaenda vyema kwa usawa .

"Viongozi wote Wa halmashauri zote za mkoa Wa Arusha watasimama imara kuhakikisha zoezi hili limekamilika ,tumegundua wananchi wengi walijiandikisha na hawajapata vitambulisho wala namba ila wanahakikisha watafanya Kazi usiku na mchana wanapata namba Na zoezi limeisha salama" alisema Gambo.

Alisema katika kuhakikisha Zoezi linaenda linaisha haraka wataongeza eafanyakazi Wa Nida ambapo alisema watatumia vijana Wa JKT ili kuweza kukamilisha zoezi hili

Naye meneja Wa mawasiliano Kanda ya kaskazini (TCRA) Muhandisi Imelda Salim alisema kuwa kufuatia zoezi la pamoja la usajili Wa namba za simu kwa alama za vidole ambalo limeratibiwa na Mkuu Wa mkoa kufuatia agizo la mh Rais John Magufuli kusogeza mbele zoezi la kusajili namba za simu kwa alama za vidole waliamua kusogeza kwa ukaribu zaidi huduma hii.

Alisema kuwa wao kama TCRA kwa kushirikiana na taasisi zingine za Nida pamoja na makampuni ya simu wamekubaliana kushirikiana ili kukamilisha maelekezo yaliotolewa Rais ,ambapo alisema wa zoezi hili limeanza katika halmashauri ya jiji la Arusha na wataendeleza katika halmashauri zote ili kila mwananchi ambae ajajiandikisha waweze kujiandikisha na kusajili namba yake ya simu.

Alibainisha kuwa Kunachangamoto ambayo imejitokeza Wananchi wengine wakienda kujisajili laini zao kwa alama za vidole wanakuta vidole vyao havimechi sasa tumetoa maagizo iwapo mwananchi wakienda tatizo hili likimkuta aache taarifa zake apo na namba ya simu mtoa huduma atapeleka hizo taarifa Nida na zitafanyiwa Kazi na tutampigia kumpa mrejesho.










from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2tzppcs
via

Post a Comment

0 Comments