Ticker

10/recent/ticker-posts

walimu vinara wa mapenzi shuleni kukiona

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Evance Nachimbinya
 
NA YEREMIAS NGERANGERA…NAMTUMBO. 

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Evance Nachimbinya amesema hatawavumilia walimu wanaosababisha migogoro mashuleni ambayo chanzo chake ni mapenzi kati ya mwalimu na mke wa mwalimu mwenzake na mwalimu na mwanafunzi wake. 

Nachimbinya aliyasema hayo kwenye kikao kazi cha wilaya ya Namtumbo kupitiia changamoto na namna ya kuzitatua, lakini pia kuhimiza utendaji kazi wa watumishi wa umma upande wa walimu ili kuleta ufanisi katika kazi ya ufundishaji. 

Kikao hicho kilikuwa ni cha walimu wakuu wa shule za msingi zote za wilaya ya Namtumbo pamoja na wakuu wa shule zote za sekondari za serikali na zile za mashirika ya dini na binafsi kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Nasuli. 

Aidha mkurugenzi wa Halmashauri aliwahakikishia walimu hao kuwa ipo migogoro iliyosababisha shule kutotulia ambayo ofisi yake imesuluhisha ni migogoro ambayo ilitokana na maswala ya mapenzi katika vituo vya kazi na kuhaidi kutovumulia walimu wanaosababisha migogoro ya namna hiyo mashuleni. 

Aden Nchimbi katibu tawala wa wilaya ya Namtumbo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho pamoja na mambo mengine alitumia pia kuwahatarisha walimu hao kuacha kujihusisha na maswala ya mapenzi yasiosahihi akimanisha kuwa kufanya mapenzi na mtu ambaye hujapata idhini ya kufanya naye mapenzi hayo ni hatari kupoteza kazi . 

Hata hivyo bwana Aden alifafanua kuwa adhabu ya kufanya mapenzi na mtu  asiyesahihi inaanza hapapa duniani kwa kuanza na kifungo jela na kadiri ya maandiko ya kitabu cha biblia amri ya kutamani mwanamke asiyemke wako ni ya sita amri hii imewekewa nyota kwa kuwa adhabu zinaaza hapahapa duniani huku amri zingine zimebaki kuwa utapata dhambi na utahukumiwa baada ya kufa alisema katibu tawala huyo. 

Amosi Mapunda mkuu wa shule ya Sekondari Nasuli alipongeza kuwepo kwa kikao hicho ambacho kwa yeye alidai ni kikao cha kukumbushana taratibu za kazi na kusimamia misingi ya taaluma ya ualimu badala ya mambo mengine katika mazingira ya shule 

Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma inajumla ya shule za sekondari 31 ikiwa za serikali 24 mashirika ya dini 6 na binafsi 1 huku shule za msingi 111 za serikali 109 za mashirika ya dini 1 na binafsi 1.



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/37U540o
via

Post a Comment

0 Comments