Ticker

10/recent/ticker-posts

WAFANYAKAZI WATATU, WAFANYABIASHARA WATATU KIZIMBANI KWA KWA TUHUMA ZA WIZI

Wafanyakazi watatu wa Kampuni ya Kamaka Ltd na wafanyabiashara watatu  wakiingia katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  jijini Dar es Salaam leo wakikabiliwa na mashtaka manne ikiwemo la wizi wa vida vya ujenzi vya zaidi ya sh. Milioni 400.

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
WAFANYAKAZI watatu wa Kampuni ya Kamaka Ltd na wafanyabiashara watatu wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka manne ikiwemo la wizi wa vida vya ujenzi vya zaidi ya sh. Milioni 400.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto amewataja wafanyakazi hao kuwa ni, watunza stoo, Salum Chemba (36) msaidizi wake Seleman Kambongo (34) na Mlinzi Japhet  Angelo (53). Wengine ni wafanyabiashara Benson William (48), Miraji Kombe (32) na Joseph Said (50).

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba imedaiwa kati ya mwaka 2015 na Desemba 14, 2019 huko Mabibo,  jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Chemba, Kambogo na Japhet wakiwa waajiriwa wa kampuni hiyo, waliiba vifaa mbalimbali vya ujenzi kwa kutumia nafasi zao za kazi vikiwa na thamani ya Sh. 438,012,180 Mali ya Kampuni ya Kamaka Ltd.

Katika shtaka la pili, imedaiwa, Desemba 19,  2019 eneo la Tabata Dampo washtakiwa William na Kombe na Said walipokea vifaa mbalimbali vya ujenzi huku wakijua kuwa vifaa hivyo ni mali ya wizi.

Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na wameachiwa huru kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama iliwataka kuwa na wadhamini wawili kila mmoja ambao watasaini Bondi ya sh. Milioni 50 na kati ya hao mdhamini mmoja anapaswa kutoa fedha taslimu sh. Milioni 50 ama kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo ya pesa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 27,mwaka huu.
Hata hivyo, mshtakiwa wa nne na wa sita walitimiza masharti hayo wako nje kwa dhamana na wengine wamepelekwa mahabusu.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Rehp8J
via

Post a Comment

0 Comments