WACHINA WASHEHEREKEA MWAKA MPYA WA KICHINA 2020 JIJINI DAR, KISWAHILI CHATHAMINIWA

  Masama Blog      
LUGHA ya kiswahili ni Lugha mojawapo inayothaminiwa sana na vijawa wa kichina hasa wafanyakazi wa taasisi China.

Hayo yameelezwa na Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke wakati wa kusheherekea mwaka mpya wa kichina 2020. Sherehe zilizo fanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Katika kusheherekea Mwaka mpya wa kichina wa 2020 walitumbuiza michezo pamoja na ngoma mbalimbali za kichina na kushiriki kikundi cha ngoma za asili kutoka hapa nchini huku kukiwa na wasanii washindi wa shindano la kusaka vipaji la BSS na kuimba nyimbo kadhaa.

 Balozi Wang Keng amesema kuwa licha ya lugha ya kiswahili kutawala katika bara la Afrika, nchini China kuna vyuo vikuu vinne vinavyofundisha kozi ya Lugha ya Kiswahili.

Hata hivyo Wang Ke amesema kuwa kila mwaka wanafunzi 10, kutoka nchini China na kuja hapa nchini katika chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kusoma Kozi ya Kiswahili.

"Wanafunzi 10 wa china huja Tanzania kusoma kiswahili katika chuo kikuu cha Dar es Salaam kila mwaka".

Katika kubadilishana katika elimu kwa nchini hizi mbili ushirikiano umezidi kuimarika huku ikitoa ufadhiri wa masomo kwa nafasi elfu mbili na fursa zaidi ya elfu sita za mafunzo ya ufundi nchini china.

Na upande wa hapa nchini China imefungua taasisi ya Confucius na madarasa mawili ya Confucius ambayo wanafundisha wanafunzi wa kitanzania utamaduni wa china na lugha ya Kichina.

Hata hivyo Balozi Wang Ke amesema kuwa wanakaribia kuanza mwaka wa panya kwani katika wanyama 12 nchini china panya huashiria akili na ustadi pia huashiria uboreshaji binafsi katika magumu.

Balozi Wang Ke katika Mwaka wa panya anatuma salamu za mafanikio makubwa katika ukuaji wa uchumi na uboreshaji wa viwango vya maisha ya watu na kuendelea kudumisha amani na maendeleo endelevu.
 Moja ya watumbuizaji wa kichina akifanya yake katika kusheherekea mwaka mpya wa kichina jijini Dar es Salaam.
 Viongozi Malimbali wa hapa nchini nao walikuwepo katika sherehe za mwaka mpya wa kichina zilizofanyika jijini Dar es Salaam.
 Suleimani Kova akiangalia maigizo na ngoma za asili katika kusheherekea Mwaka mpya wa kichina, katika sherehe zilizofanyika jijini Dar es Salaam.


 Baadhi ya wananchi wakiangalia ngoma za asili za China wakati wa kusheherekea mwaka mpya wa kichina jijini Dar es Salaam.
 Washehereshaji wa sherehe ya mwaka mpya wa kichina, sherehe iliyofanyika jijini dar es Salaam katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere.

 Watoto wa kichina wakicheza Mchezo wa ngoma ya asili ya china wakati wa kusheherekea mwaka mpya wa kichina wa 2020 jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere. Kikundi cha Sanaa cha China wakicheza Mchezo wa nyani katika sherehe za Mwaka Mpya wa kichina 2020 jijini Dar es Salaam.


 Baadhi ya washindi wa shindano la kusaka vipaji la BSS wakitum uiza wakati wa kusheherekea mwaka mpya wa kichina jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya watanzania na wachina wakicheza ngoma ya asili ya kichina katika kusheherekea mwaka mpya wa kichina wa 2020 jijini Dar es Salaam.Mtumbuizaji wa kichina anayeweza kubadilisha sura yake kwa mara kadhaa na kuwa na rani mbalimbali katika sura yake na hata kuwa na michoro katika sura yake.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/368iNiS
via
logoblog

Thanks for reading WACHINA WASHEHEREKEA MWAKA MPYA WA KICHINA 2020 JIJINI DAR, KISWAHILI CHATHAMINIWA

Previous
« Prev Post