VULLU AHIMIZA WANANCHI KUJITOKEZA KATIKA ZOEZI LA UBIRESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

  Masama Blog      ****************************
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani Zaynab Matitu Vullu, amewaasa viongozi wa kisiasa na wa Serikali kuwahimiza wananchi kujitokeza katika zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura.
Lengo kubwa ni kwa wananchi hao kuweza kishiriki zoezi la kupiga kura katika chaguzi zinazotarajia kufanyika mwaka huu 2020, kuanzia Udiwani, Ubunge na Rais.
Vullu alitoa rai hiyo katika Kijiji cha Kisangile, Kata ya Marui wilaya ya Kisarawe akiwa kwenye ziara iliyoratibiwa na Jumuiya ya Wanawake ya (UWT) ya chama hicho.
Alisema ,zoezi la uboreshaji wa daftari la wapigakura linalotaraji kuanza Feb 2 litalodumu kwa siku saba, limeandaliwa na serikali kwa lengo la kuwapatia nafasi wa-Tanzania kuhakiki majina yao kwenye daftari hilo.
“Serikali imeandaa daftari hilo kwa lengo la kuwapatia fursa wananchi kuhakiki majina yao, hatua itayomwezesha mlengwa kupara nafasi ya kushiriki zoezi la kupiga kura kwa kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi,” alisema Vullu.
Aidha alitolea ufafanuzi wa tofauti wa kadi ya kupigia kura na kitambulisho cha taifa, baada ya mkazi aliyejitambulisha kwa jina la Khalfan Mussa kuhoji utofauti wa kadi hiyo ya kupigiakura na kitambulisho cha taifa.
Nae Sophia ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya hiyo alielezea, zoezi hilo litakalodumu kwa wiki moja halitakuwa na muda wa nyongeza, hivyo amewaasa wana-Kisarawe kuchangamkia fufsa hiyo ili waweze kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa.
Diwani wa Kata hiyo Salehe Mfaume alieleza,wamejipanga kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa mafanikio makubwa.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2RRoVqr
via
logoblog

Thanks for reading VULLU AHIMIZA WANANCHI KUJITOKEZA KATIKA ZOEZI LA UBIRESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

Previous
« Prev Post