Uwekezaji wa Serikali Hospitali Mloganzila ni Mkubwa -Mkurugenzi Mtendaji Magandi

  Masama Blog      
 Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Redemtha Matindi akinesha moja chumba ambayo wataanza kutoa huduma za upandikizaji wa uroto.
Mashine ya Mapafu  iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila.
 Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Daktari Bingwa Julieth Magandi akizungumza na waandishi habari pamoja na Timu ya maafisa habari wa Taasisi zilizo chini ya  Wizara ya Afya,Maendeleo Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kuangalia mafanikio ya sekta ya afya inayokwenda na Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya afya ambayo ilifika katika hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.
 Mashine ya MRI iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila.
 Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Catharine Sungura akizungumza na waandishi wa  habari na Maafisa wa Habari wa Taasisi zilizo Chini ya Wizara hiyo katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya afya kuangalia mafanikio ya uwekezaji wa Serikali katika sekta hiyo katika hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.
 Mashine za mazoezi Tiba zilizopo katika hospitali ya Mloganzila.
 Moja ya chumba cha kupandikiza uroto ambayo huduma hiyo itaanza kutolewa katika hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.
 Afisa Habari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Neema Mwangomo akizungumza na waandishi habari pamoja na Timu ya maafisa habari wa Taasisi zilizo Chini ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto wakati walipofika kuangalia mafanikio ya sekta ya afya ya uwekezaji wa Serikali katika kipindi cha miaka minne kwa Kampeni ya maafisa hao ya Tumeboresha Sekta ya Afya.

Uwekezaji wa Serikali Hospitali Mloganzila ni Mkubwa -Mkurugenzi Mtendaji Magandi

Na Chalila Kibuda,Globu ya JamiiSerikali kwa kutambua umhimu wa afya kwa Wananchi wake imewekeza nguvu Hospitali ya Taifa  Muhimbili-Mloganzila ikiwa ni pamoja kuweka rasiliamali ya madaktari bingwa na wabobezi katika nyanja mbalimbali hospitalini hapo.

Akizungumza na waandishi wa Habari pamoja na Timu ya Maafisa Habari wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Daktari Bingwa Julieth Magandi amesema Hospitali ya Mloganzila imewekezwa kwenye miundombinu pamoja na mashine ili kurahisisha utoaji huduma kwa wagonwa hali ambayo  serikali imepunguza gharama ya kutibu wananchi wake nje ya nchi.

Amesema katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt.John Pombe Magufuli imeweka sekta ya afya kipaumbele kwa kutenga fedha nyingi katika sekta  hiyo kwa kuondoa changamoto ya magonjwa yaliyokuwa yakifanyika nje ya nchi kufanyika sasa katika hospitali ya Mloganzila.

Hata hivyo amesema kuwa wanatarajia kuanza kupandikiza uroto katika uti wa mgongo kwani miundombinu yake hiyo iko tayari ikiwa ni Pamoja na kuimarisha chumba cha uangalizi Maalum (ICU) ambapo wanatarajia kupata  madaktari Bingwa  na wabobezi wanne kutoka nchini Cuba pamoja na wauguzi wa wawili.

Magandi amesema kuwa katika mpango wa Hospitali ya Mloganzila wataanza kutoa huduma ya kuondoa mawe kwenye figo kwani tatizo hilo lipo hivyo kama Hospitali tunawajibika kuwatibu wananchi wetu.
"Serikali imefanya kazi kubwa katika hospitali ya Mloganzila katika uwekezaji wa miundombinu na mashine tunawajibu wa kutoa huduma Bora za afya kwa mazingira yaliyopo hospitalini hapa kwa kuendana na viwango baadhi nchi zilizoendelea"amesema Magandi.

Hata hivyo amesema kuwa kuwa wanauwezo wa kufanya upasuaji huku wengine wakiangali sehemu nyingine kutokana na mfumo ulioko katika hospitali hapo.

Amesema ikiwa ni pamoja na uwekezaji huo katika Teknolojia ya habari  ya Mawasiliano wamekuwa na mifumo mbalimbali ambayo imerahisisha utoaji wa Huduma kwa wagonwa kwani wanaweza kutuma kitu kinachohusiana na matibabu kwenda sehemu nyingine ya ndani ya hospitali  kwa njia ya mtandao.from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2tlCZQI
via
logoblog

Thanks for reading Uwekezaji wa Serikali Hospitali Mloganzila ni Mkubwa -Mkurugenzi Mtendaji Magandi

Previous
« Prev Post