Ticker

10/recent/ticker-posts

UTURUKI YASAINI MKATABA UENDESHAJI SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ZILIZO CHINI YA TAASISI YA SOS TANZANIA

Na,Jusline Marco:Arusha

Nchi ya Uturuki imesaini mkataba wa uendeshaji na usimamizi wa shule za msingi na sekondari zilizo chini ya taasisi ya SOS Tanzania ili kuweza kuendeleza sekta ya elimu nchini.

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kusaini mkataba huo ulioambatana na ziara ya kutembelea watoto wanaotoka katika mazingira magumu SOS viillage iliyoko Wilayani Arumeru Mkoani Arusha,Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Ali Davitoglu amesema kuwa nchi ya Uturuki imeamua kuwekeza katika sekta hiyo kwa ajili ya kuboresha elimu kwa watoto wa kitanzania wanaoishi kwenye mazingira magumu hususani wa jamii ya kifugaji.

Aidha amesema uwekezaji huo umelenga kuinua kiwango cha elimu kwa watoto wa kitanzania ili waweze kupata mafanikio yatokanato na elimu bora.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya taasisi ya SOS Bi.Merry Nagu amesema kuwa uwekezaji huo utahakikisha ubora wa elimu kwa watoto unatolewa ili kuweza kujikomboa na umaskini.

Naye Kaimu Afisa elimu Wilaya ya Arusha Grace Massawe amewatakata waliowekeza katika sekta hiyo kuhakikisha wanazingatia mtaala wa kitanzania unaotumika katika elimu ili kuweza kujenga jamii iliyo bora.

 Balozi wa Uturuki nchini Ali Davutoglu katikati akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa taasisi ya SOS Village Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36wV8cY
via

Post a Comment

0 Comments