Na Yeremias Ngerangera
Utalii na uwindaji wa kitalii katika jumuiyya ya Mbarang’andu umeanza kupaa baada ya musimu wa uwindaji wa kitalii kuanza julai mosi mwaka jana 2019 katika jumuiya hiyo.
Afisa wanyamapori wa Halmashauri ya wilaya Namtumbo Ernest Nombo katika taarifa yake alisema utalii wa uwindaji na utalii wa kuona umeongezeka katika musimu wa julai hadi desemba 2019 ikilinganishwa na misimu miwili ya nyuma.
Bwana Nombo alidai kuongezeka kwa utalii katika jumuiya hiyo kumetokana na uhifadhi wa wanyama kukiendana na ongezeko la wanyama wanaovutia watalii kwenda kuwaona na kuomba kibali cha kuwinda.
Aidha bwana Nombo amesema katika musimu wa Julai mpaka desemba 2019 jumuiya ya Hifadhi wanyamapori kwa jamii (WMA) ya mbarang”andu inastahili kupata gawio la fedha kutoka TAWA kiasi cha dola za marekani 53,817.5 na Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kupata gawio kiasi cha dola za marekani 8,807.5.
Ofisa Ardhi na maliasili wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Saimon Sambalu katika taarifa hiyo alidai kanuni za jumuiya za uhifadhi wanyamapori (WMAs) za mwaka 2018 kifungu cha 72(1) na (2) (b) vinaeleza kuwa asilimia 50 ya mapato ya mwaka yatokanayo na uwindaji wa kitalii kwenye WMA lazima yapelekwe katika vijiji vinavyounda jumuiya husika .
Bwana Sambalu katika tarifa hiyo alisema asilimia 50 ya dola za kimarekani 53,817.5 ni sawa na dola za kimarekani 26,908.75 ambapo kijiji cha kitanda ,Nambecha,Likuyuseka ,Songambele,Mchomoro ,Kilimasera na Mtelamwahi vitapata kiasi cha dola za marekani 3,844.10 kila kijiji.
Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ina jumla ya jumuiya ya Hifadhi za wanyamapori za jamii(WMAs)tatu ikiwemo ya Kisungule,Kimbanda pamoja na Mbarang”andu ambayo inaonekana kuwa na idadi kubwa ya utalii katika msimu wa julai mpaka desema 2019.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/38cJd47
via
0 Comments