UONGOZI KLABU YA SIMBA WASIKITISHWA NA KAULI YA MCHEZAJI WA YANGA RAMADHAN KABWILI ...WAACHA TFF ICHUNGUZE,ICHUKUE HATUA KALI IWE FUNDISHO

  Masama Blog      
Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii


KLABU ya Simba imepokea kwa masikitiko kauli ya mchezaji Ramadhan Kabwili aliyoitoa Januari 27 mwaka 2020 kwenye kituo cha Radi cha East Africa cha  jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba Senzo Mbatha amesema kuwa kauli za aina hiyo kutoka kwa wachezaji ni za kuchukiza na sio za heshima ambazo zinaashiria upangaji wa matokeo ya mechi kama ilivyotuhumiwa na mchezaji huyo ambazo Klabu ya Simba inazipinga na kuzikemea vikali.

Amesema kauli hizo zina madhara makubwa kwenye uadilifu wa Klabu ya Simba na viongozi wake,uadilifu na heshima ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) kwa ujumla unawekwa mashakamani kama kauli za namna hiyo hatzitachukukuliwa hatua stahiki.

"Klabu ya Simba inafurahishwa na hatua za haraka zilizochukuliwa na TFF dhidi ya kauli kama hizi kwa vyombo husika ,klabu ya Simba inaamini kwamba jambo hili liko kwenye mikono ya vyombo husika na litachukuliwa hatua stahiki kwa haraka,"amesema Mbatha.

Ameongeza Klabu ya Simba inaendelea kuweka juhudi zake kwenye miradi yake na ratiba za Ligi kuu pamoja na Kombe la Shirikisho la Azam .Pia wanaendelea kujitayarisha tayari kwa kukabili mechi za michuano iliyopo mbele yao ikiwa ni pamoja  na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa timu na benchi la ufundi.

Wakati wa Simba ikitoa msimamo huo ,baadhi ya wadau ambao wamezungumzia na Michuzi Globu ya jamii, leo jijini Dar es Salaam wamesema  kuwa kwasababu jambo hilo TFF wameshaonesha nia ya kuchukua hatua,wanaona ni vema wakaendelea nalo iwapo itabainika hatua kali zichukuliwe iwe klabu au aliyetoa taarifa hiyo ili iwe fundisho kwa klabu au wachezaji.

Pia wameomba baada ya ,uchunguzi kufanyika ni vema taarifa zinatolewa hadharani ili wadau na wapenzi wa soka wajue. Hata hivyo wadau wengine wamesema Rais wa Shiriko la Mpira wa Miguu Duniani(FIFA)aliyepo sasa Gianni Infantino hataki kabisa masahara kwenye upangaji matokeo na rushwa katika mchezo huo.Hivyo wadau wameshauri ni vema suala hilo likashughulikiwa kwa umakini mkubwa kwani linamadhara kwa Ligi yetu, wadau wa soka,vilabu na wachezaji kwa ujumla.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Rw6KHQ
via
logoblog

Thanks for reading UONGOZI KLABU YA SIMBA WASIKITISHWA NA KAULI YA MCHEZAJI WA YANGA RAMADHAN KABWILI ...WAACHA TFF ICHUNGUZE,ICHUKUE HATUA KALI IWE FUNDISHO

Previous
« Prev Post