UJENZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ZIMAMOTO KUKAMILIKA JANUARI 31

  Masama Blog      
Charles James, Michuzi TV

WIZARA ya Mambo ya Ndani imesema Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania (CGF), Thobias Andengenye atahamia Makao Makuu ya Nchi, Dodoma ifikapo Fabruari 10, mwaka huu.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kahilima wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dodoma leo.

Akizungumza na wandishi wa habari baada ya kukagua maendeleo ya jengo hilo, Kahilima amesema ujenzi huo umefikia asilimia 90 hivyo wana matumaini utakamilika katika muda uliopangwa na Jeshi hilo litakabidhiwa jengo lao ifikapo Januari 31, mwaka huu.

"  Tunamshukuru Rais Dk John Magufuli ambaye alitupatia Sh Milioni 910 kwa ajili ya ujenzi wa jengo hili ambalo hadi kukamilika kwake litagharimu Sh Bilioni 2.6 ambapo Februari 10 tunaamini kabisa Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji, Makamishna wake na wasaidizi wengine watahamia hapa Dodoma," Amesema Kahilima.

Mradi huo unasimamiwa na Mrakibu wa Jeshi la Polisi nchini, Costantine Kiwote ambaye amesema mradi huo ulianza februari 4,2019 na hadi kukamilika utagharimu kiasi cha Sh Bilioni 2.6, ambapo kati ya hizo Sh53 milioni zimetumika kwenye mfumo wa maji machafu na tayari zilimeshalipwa Duwasa.

Aidha ameshukuru wizara kwa namna ambavyo imetoa ushirikiano kwao kwenye kipindi hiki cga ujenzi wa mradi huo ambapo amesema licha ya kujitokeza kwa baadhi ya changamoto wao walizibadili na kuzifanya kuwa fursa na wanaamini watakamilisha ujenzi huo katika muda uliopangwa.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kahilima akizungumza na baadhi ya maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji alipoenda kukagua ujenzi wa mradi wa jengo la Makao Makuu ya Jeshi hilo leo jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Ramadhani Kahilima akitoka kwenye jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma alipoenda kukagua maendeleo ya ujenzi wake.
 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2QjREEG
via
logoblog

Thanks for reading UJENZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ZIMAMOTO KUKAMILIKA JANUARI 31

Previous
« Prev Post