UJENZI JENGO LA UMOJA WA POSTA AFRIKA (PAPU) KUKAMILIKA NDANI YA MIEZI 30

  Masama Blog      Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe ( wa kwanza kushoto) akiweka rasmi jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la ofisi za makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika wakati wa Maadhimisho ya Miaka 40 ya Umoja huo yalifanyika januari 18/2020 jijini Arusha. Wanaoshuhudia kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe,Katibu mkuu mtendaji wa PAPU Afrika Younouss Djibrine,Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,pamoja na Waheshimiwa Mawaziri wa nchi mbalimbali wakishuhudia utayari wa uwekekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la PAPU jijini Arusha jana wakati wa Maadhimisho ya miaka 40 ya Umoja wa Posta Afrika
Naibu waziri wa Mambo ya nje ushirikiano wa kimataifa na kikanda Damas Ndumbaro akisoma maneno yaliyoandikwa kwenye jiwe la msingi mbele ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akipongezana na Mkurugenzi mkuu mtendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Mhandisi James Kilaba mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la ofisi za makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika wakati wa Maadhimisho ya Miaka 40 ya Umoja huo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe ( wa kwanza kushoto) akiweka rasmi jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la ofisi za makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika wakati wa Maadhimisho ya Miaka 40 ya Umoja huo yalifanyika januari 18/2020 jijini Arusha. Wanaoshuhudia kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo

Na.Vero Ignatus,Arusha

Jumla ya shilingi bilioni 33.58 kutumika kwaajili ya ujenzi wa jengo la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) ambapo unatekelezwa kwa ubia kati ya serikali ya Jamhuri ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA na Umoja nchi wanachama wa Umoja wa posta Afrika (PAPU)ambapo unatazamiwa kukamilika ndani ya miezi 30 kuanzia sasa.

Uwepo huo wa jengo la PAPU nchini Tanzania kutakuwa na manufaa mamkubwa kwa nchi kwasababu kutaongeza nafasi za Taasisi hiyo ya kimataifa sambamba na kuratibu shughuli ya sekta ya posta Afrika utaongezeka .

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Isack Aloyce Kamwelwe katika hafla ta uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la makao makuu ya Umoja wa Posta Afrika( PAPU ) ambapo alisema kuwa jengo hilo litatumika kama kitega uchumi cha kuleta maendeleo katika kutoa ajira kuboresha mandhari ya jiji la Arusha sambamba na kudumisha heshima ya nchi ya Tanzania,mbele ya nchi wanachama na duniani kote

''Na tukaenzi jitihada za na fikra za baba wa Taifa Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere Rais wa Kwanza wa Jamuhuri ya Muuungano wa Tanzania kwa Tanzania na Afrika''Alisema

Mhe.Kamwelwe alimetoa wito kwa watanzania na kuwataka kuchangamkia fursa kuchangamkia fursa ya ajira pindi mahitaji yatakapotokea pia amewaomba wale watakaoajiriwa kuwa waaminifu katika utendaji huo ili mwisho wa siku lipatikane jengo lenye ubora sawa na thamani ya fedha iliyotumika.

''Kwa mradi huu mkubwa na utekelezaji wake unafanyika hapa nchini ninaamini wataalamu wengi watahitajika tafadhali nawaombeni msihujumu mradi huu na badala yake mkawe walinzi wa mradi huu''alisema

Aidha ameushukuru uongozi wa mkoa wa Arusha ukiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha mhe.Mrisho Gambo kwa kwa kukubali kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya miaka 40 ya Umoja wa Posta Afrika

Kwa upande wake Mtendaji mkuu wa Umoja wa posta duniani amesema kuwa jengo hilo litakapomalizika na kuanza kufanya kazi wataangalia ni namna ambavyo wanaweza kuleta chuo cha mafunzo ya posta hapa nchini Tanzania

Kwa upande wake amesema Naibu waziri wa Mambo ya nje ushirikiano wa kimataifa na kikanda Damas Ndumbaro jambo kubwa haswa katika uwekaji wa jiwe hilo la msingi ni kuimarisha Umoja wa Kimataifa kwani PAPU ni chombo cha kimataifa ni chombo ambacho kinaunganisha Tanzania nanchi nyingine Barani Afrika pamoja na nchi nyingine ulimwenguni

Amesema kuwa uwepo wa PAPU ni uthibitisho tosha kwamba kwa miaka 40 iliyopita tangia kuanzishwa kwake mahusiano na ushirikiano wa kimataifa ni mzuri na wataendelea kuumarisha zaidi

Naye mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewahakikishia PAPU kuwa serikali ngazi ya mkoa wataendelea kutoa ushirikiano kwa Wizara ya ujenzi na Mawasiliano na Uchukuzi Taasisi zote kutoka nje ya Tanzania kuhakikisha kwamba mipango na miradi yote ambayo inaletwa mkoani hapo inatekelezwa kwa kadri ambavyo inaonekana inafaa


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2v5CZoF
via
logoblog

Thanks for reading UJENZI JENGO LA UMOJA WA POSTA AFRIKA (PAPU) KUKAMILIKA NDANI YA MIEZI 30

Previous
« Prev Post