Ticker

10/recent/ticker-posts

UFILIPINO YAAANZA KUWAONDOA RAIA WAKE IRAQ

Serikali ya Ufilipino imewamuru Raia wake kutoka Iraq huku walinzi wa Pwani wakisema wanapeleka meli kwenda Mashariki ya Kati ili kuwapeleka Raia wake kwenye usalama ikiwa hali ya uadui kati ya Marekani na Iran inaendelea kuwa mbaya
-
Idara ya Mambo ya nje ya Ufilipino imesema serikali imeongeza kiwango cha tahadhari nchini Iraq kwa kiwango cha juu zaidi, na kuwahitaji Wafilipino kuondoka nchini humo kutokana na hatari kubwa za kiusalama. Wafilipino wanaweza kuondoka peke yao au kusindikizwa kwa msaada wa waajiri wao au serikali ya Ufilipino
-
Mataifa mengine ya Asia yaliyo na idadi kubwa ya Raia nchini humo yanaweza kufikia maamuzi kama hayo baada ya Iran kurusha makombora katika vikosi vya Marekani nchini Iraq na kuongezeka kwa uadui
-
India, ambayo ina idadi kubwa ya wafanyakazi katika Mashariki ya Kati, iliwashauri Raia wake waepuke safari sisizo za muhimu kwenda Iraq. Pia, iliwahimiza Raia wake wanaoishi Iraq kuendelea kuwa macho na kujiepusha na safari ndani ya nchi


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2T2NB1r
via

Post a Comment

0 Comments