Ticker

10/recent/ticker-posts

TUSHIRIKIANE KUPIGIA MBIU LUGHA YA KISWAHILI :PROF.MWAMFUPE

Muasisi wa wazo kla kuandika kitabu cha Koja Koja la Taaluma za Insia ambaye pia ni Mhariri wa kitabu hicho Dkt.Athuman Ponera ,ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi katika chuo kikuu cha kumbukumbu ya Mwal.Nyerere Kampasi ya Zanzibar,akiwa na Mhadiri wa Idara ya Kiswahili Chuo kikuu cha Dodoma Dkt.Zuhura Badru ambaye naye alikuwa mhariri mwenza wa kitabu hicho cha Koja walkiwa katika picha ya pamoja na Profesa Madumulla.



Profesa Joshua Samwel Madumulla akikabidhiwa zawadi na mhadhiri msaidizi taaluma za kiswahili chuo kikuu ca Dodoma



Profesa Joshua Samwel Madumulla akikabidhiwa zawadi na mhadhiri msaidizi taaluma za kiswahili chuo kikuu Dodoma


Mhadhiri wa Chuo Kikuu Udom akimkabidhi Profesa Madumulla zawadi.
Profesa Joshua Samwel Madumulla akipeana mikono na Dkt.Zuhura Badru mara baada ya kumkabidhiwa zawa iliyoandaliwa na Idara ya Kiswahili chuo kikuu cha Dodoma .
Meya wa Jiji la Dodoma Profesa Davis akikionyesha kitabu mara baada ya kukata utepe.
Makabidhiano ya fedha mara baada ya mauzo ambapo ziliuzwa zaidi ya nakala 70



Mgeni Rasmi katika akikata utepe katika Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Koja la Taaluma za Insia kilichochapishwa kwa heshima ya Profesa Joshua Samwel Madumulla
Meya wa Jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe akimkabidhi kitabu Profesa Joshua Samwel Madumulla kilichoandaliwa kwa heshima yake katika chuo kikuu cha Dodoma kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kukuza,kuenzi na kuendeleza lugha ya kiswahili katika chuo kikuu ca dodoma ,tanzania na hata nchi jirani.
Meya wa Jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe akimpongeza Profesa Joshua Samwel Madumulla kwa kazi kubwa aliyoifanya hadi kuandaliwa kitabu kwa heshima yake katika chuo kikuu cha Dodoma kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kukuza,kuenzi lugha ya kiswahili.
Profesa Albino Tenge wa Rasi ya Ndaki ya Insia na Sayansi ya jamii Chuo Kikuu cha Dodoma akitoa neno katika Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Koja la Taaluma za Insia kilichochapishwa kwa heshima ya Profesa Joshua Samwel Madumulla
Pofesa Joshua Samwel Madumulla akiwa anazungumza na wageni waalikwa katika Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Koja la Taaluma za Insia kilichochapishwa kwa heshima yake iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Muwakilishi wa Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Dodoma Profesa Mwegoha akitoa neno katika Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Koja la Taaluma za Insia kilichochapishwa kwa heshima ya Profesa Joshua Samwel Madumulla

Mmoja wa wanafunzi wa Profesa Joshua Madumulla Dkt.Abdulimalick Feruz akichangamsha ubongo wa wageni waliohudhuria Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Koja la Taaluma za Insia kilichochapishwa kwa heshima ya Profesa Joshua Samwel Madumulla
Muwakilishi kutoka Chama cha kusanifu Ushairi Tanzania Bi.Asia Kulastara akisoma shairi katika Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Koja la Taaluma za Insia kilichochapishwa kwa heshima ya Profesa Joshua Samwel Madumulla
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanataaluma waChuo Kikuu cha Dodoma Dkt.Julius Ntwenya akitoa neno katika hafla hiyo
Wa kwanza kushoto ni Profesa Hermans Mwansoko akiwa pamoja na Profesa Joshua Samwel Madumulla,katika ukumbi wa Ukumbi wa Mihadhara Chuo Kikuu cha Dodoma.

Wa kwanza kushoto ni Profesa Hermans Mwansoko akiwa pamoja na Profesa Joshua Samwel Madumulla Meya wa Jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe (anayeandika),wa kwanza kulia ni Dr.Athuman Ponera
Wa kwanza kulia Mgeni Rasmi Meya wa Jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe (anayeandika) (katikati)Profesa Joshua Samwel Madumulla pamoja na Profesa Hermans Mwansoko
Wa kwanza kulia Mgeni Rasmi Meya wa Jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe (anayeandika) (katikati)Profesa Joshua Samwel Madumulla pamoja na Profesa Hermans Mwansoko


Baadhi ya washiriki waliojitokeza kuhudhuria Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Koja la Taaluma za Insia kilichochapishwa kwa heshima ya Profesa Joshua Samwel Madumulla



Picha ya pamoja ya baadhi ya washiriki katika Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Koja la Taaluma za Insia kilichochapishwa kwa heshima ya Profesa Joshua Samwel Madumulla



Picha ya pamoja ya baadhi ya wanafunzi katika Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Koja la Taaluma za Insia kilichochapishwa kwa heshima ya Profesa Joshua Samwel Madumulla




Na,Vero Ignatus,Dodoma.

Uzinduzi wa kitabu cha Koja la Taaluma za Insia kilichotolewa kwa heshima ya Profesa Joshua Samwel Madumulla umefanyika Jijini Dodoma katika Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ukiwa na lengo la kuenzi kazi za wataalam wa lugha ya kiswahili na kutambua mchango wao katika kukuza lugha hiyo

Akizungumza katika uzinduzi huo mgeni rasmi ambaye ni Meya wa Jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe amesema kuwa Lugha ya Kiswahili inazidi kutanuka na kwenda mipaka nchi nyingine hivyo inafungua fursa za kibiashara baina ya hizo

Profesa Mwamfupe amesema kuwa Tanzania haiwezi kuwa na viwanda vya kuzalisha kila kitu hapa nchini bali uchumi huo utakuwa umetekelezeka pale ambapo kutakuwa na ushirikiano wa kibiashara kutoka kwa mataifa mengine ambapo watu watanunua bidhaa hapa nchini hivyo lazima katikati ya mnunuzi na mnunuaji kunakuwepo na umuhimu wa matumizi ya lugha.

Muwakilishi wa makamu mkuu wa chuo cha Dodoma Profesa Mwegoha amesema heshima ya mwanataluma Pro.Joshua Mdumulla aliyopewa katika lugha ya Kiswahili itachagiza watu wengi kukipenda Kiswahili na hivyo kusambaa katika sehemu nyingi ndani ya nchi na nje ya nchi huku akitaka kuendelea kuwaenzi wanataaluma waliotumia muda wao mwingi kuitumikia jamiii kukumbukwa na kuthaminiwa sana hata watakapomaliza muda wao wa kitaaluma.

Akishukuru mara baada ya kutunukiwa andiko la kitabu cha Koja la taaluma za Insha Pro.Joshua Mdumulla alisema kuwa hapo awali walikuwa wamelala kuhusu lugha ya Kiswahili kwani waliwaachia nchi jirani wakifanya mengi kuonyesha kwamba wao ndiyo wenye Kiswahili,amesema Tanzania kwa sasa imejikita katika kuhamasisha lugha ya Kiswahili huku wakiunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli za kukuza kiswahili

Amesema kuwa anao uhakika kwamba kwa muda mfupi nchi ya Tanzania itapiga hatua kubwa sana katika kukuza na kuieneza lugha hiyo,hivyo amewahimiza watanzania kwamba washirikiane katika kukipigia mbiu lugha ya kiswahili ili kiweze kuendelea na kuenea katika dunia

Akitoa salamu kwa niaba ya wawakilishi waliowahi kuwa wanafunzi wa mtambarukiwa Prof.Madumulla ,Dkt Sanga:amesema kuwa amekuwa ni mwalimu wa pekee na heshma anayotunukiwa amestahili,kutokana na mchango wake katika lugha ya Kiswahili ambapo kwenye chou cha Dodoma idara ya Kiswahili ina madaktari wengi ambapo yeye kasimamia elimu zao na siyo kwa Dodoma tu bali Tanzania nzima.

Kwa upande wake muwakilishi kutoka Jumuiya ya wataalamu UDOM kiongozi wa Mwenyekiti wa UDOMASA Dkt.Julius Mtwenya amesema kuwa anamfananisha profesa na mama wa kitanzania ambaye anaishi maeneo yasiyokuwa na mtandao lakini bado aliendelea kuwalea Watoto katika mazingira magumu lakini aliendelea kukesha na wanafunzi bila kujali.

Katika hatua nyingine Dkt. Mtwenya amesema kuwa anamfananisha Prof. Mdumulla na viongozi wa dini ambao wanatengeneza wafuasi wengi kwasababu kila anapokutana na wanafunzi wenye shida aliweza kutatua hivyo imemfanya kumuona ni Tajiri mkubwa mwenye watu wengi

''Tutaendelea kuyaenzi na kuyaishi yale yote aliyoyaacha kwani wanataaluma kutoka Chuo kikuu cha Dodoma tunenufaika sana sana na elimu yake"alisema

Naye Mkuu wa Idara ya Kiswahili Chuo kikuu cha Dodoma Dkt.Zuhura Badru alisema kuwa Kiswahili ni lugha inayotumika katika nchi mbalimbali katika nchi za Afrika,na nchini Tanzania lugha ya kiswahili inatumika katika mawasiliano katika idara mbalimbali za serikali ikiwamo Mahakamani,Bungeni na sehemu nyingine.

Dkt.Zuhura alisema kuwa idara ya Kiswahili itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kukuza na kukienzi Kiswahili hapa nvhini na duniani pote.

Akitoa salamu kutoka ofisi ya Rasi wa Ndaki ya Insia na Sayansi za jamii ya Chuo kikuu cha Dodoma Prof.Albino Tenge wamempongeza Prof.Joshua Samwel Mdumulla kwa mchango mkubwa kwa kuendeleza na kukuza Kiswahili na kueleza kuwa ni mmoja wa waanzilishi wa chuo kikuu cha Dodoma na kusema kuwa anao utajiri wa watu wengi walipitia miknoni mwake.

Ametoa rai kwa wanafunzi waliokuwepo katika eneo husika watumie taaluma zao kwa kuacha alama katika jamii zao na kukienzi Kiswahili ili jamii iweze kutambua umhimu wa lugha hiyo.

Kwa upande wake muasisi wa wazo la kuandika koja Koja la taaluma za Insha Dkt.Ahuman Ponera amesema kuwa amesema Prof.Madumulla ni mwanataaluma adhimu katika uga wa fasihi amekuwa mstari wa mbele katika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili na fasihi kwa ujumla.

Dkt.Ponera alisema kuwa amwekuwa miongoni miongoni mwa wataalamu ambao wamekuwa na mchango mkubwa kupitia utafiti na machapisho mbalimbali katika Nyanja nyingi kama vile riwaya ya Kiswahili,fasihi ya Watoto,uandishi,uchapishaji,usomaji,uhakiki,fasihi simulizi na ujumi

Dkt. Ponera amesema kuwa mbali na hayo Prof.Madumulla amewahi kushika nyadhifa kwenye asasi mbalimbali baadhi ni amewahi kuwa mwenyekiti wa kwanza wa ukuzaji wa vitabu Tanzania (1998-2002)mwenyekiti wa kamati ya vitabu vya Watoto(1995-1999)mwenyekiti wa chama cha wasomaji Tanzania (2000 hadi sasa)Amid mshiriki,(taaluma)kituo cha Sanaa na sayansi za jamii (2000-2003)mjumbe kamati ya utafiti na uchapishaji ya utafiti na elimu ya demokrasia Tanzania reserch and education for democracy in Tanzania (REDET)ambapo alihariri machapisho kadha.

Adha amesema nyadhifa nyingine ni pamoja mkuu wa idara ya Kiswahili chou kikuu cha Dar es salaam(2004-2006)Amid skuli ya Sanaa na lugha chou kikuu cha Dodoma (2007-2012)naibu Makamu mkuu wa chuo cha taaluma chuo kikuu cha Eckernforde Tanga (2012-2019)Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Iringa(2015-2018 )vilevile ni muasisi na mwanachama,kiongozi na mlezi wa jumuiya mbalimbali zinazojihusisha na lugha za fasini,jumuiya moja wapo aliyoianzisha ni chama cha lugha na fasihi ya Kiswahili Tanzania (CHALUFAKITA)

Dkt.Ponera amesema kuwa kitabu hicho kinachoitwa Koja la Taaluma za Insia kwa kifupi maana ya jina hilo ni taji au utungo uliosheheni maswala mbalimbali yanayohusiana na taaluma za Insia.

Amefafanua maana ya Insia ni neno lililotoholewa kutoka lugha ya kiarabu ins-yaani mtu ama watu,hivyo insia linatoka kwenye neno Insia ambapo maana yake ni kuhusiana na watu.

Amesema kuwa kitabu hicho chenye kurasa 32ambazo zimegawanyika katika sura 10zenye mnyumbuliko tofautitofauti wameweza kuzalisha kopi 72 na wameuza kwa mnada na kupata jumla ya shilingi million 2.5


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2RcdadR
via

Post a Comment

0 Comments