TP MAZEMBE YAMREJESHA KUNDINI THOMAS ULIMWENGU KWA KANDARASI YA MIAKA MIWILI

  Masama Blog      
Na Yassir Simba,  Globu ya Jamii

Klabu ya Tout Puissant Mazembe (TP MAZEMBE) yenye maskani yake mjini Kamalondo, Lubumbashi katika nchi ya Jamhuri ya Demokrasia Congo kupitia mtandao wao wa kijamii wa Instagram imetangaza kurejea tena katika klabu hiyo winga wa kimataifa raia wa Tanzania Thomas Ulimwengu.

Thomas Ulimwengu mwenye umri wa miaka 27 amerejea tena mjini Lubumbashi kwa mabingwa hao mara 5 wa klabu bingwa barani Afrika mara baada ya kuingia nao mkataba wa miaka 2 kukitumika tena kikosi hicho cha wannabe hao wa Jamhuri ya Demokrasia Congo.

Ulimwengu aliondoka klabuni hapo mnamo mwaka 2016 kuelekea barani Ulaya katika kutafuta changamoto mpya katika maisha ya soka.Mnamo mwaka 2017 na 2018 alitua katika klabu ya Athletic Football Eskiltsuna ya nchini Sweden na katika miaka hiyohiyo Ulimwengu alitua tena katika klabu ya Bosnia Fc Sloboda Gorazde.

Mara baada ya kuchemesha katika soka barani Ulaya, Ulimwengu alirejea tena barani Afrika na kujiunga na ya Al Hilal ya nchini Sudan ambapo hakupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo ndipo mwaka uliofuata alijiunga na klabu ya Js Saoura ya nchini Algeria ambapo alicheza katika hatua ya makundi klabu bingwa barani Afrika.

Ulimwengu anarejea tena TP MAZEMBE  kwa lengo la kuongeza kasi na nguvu katika kikosi hicho huku akitarajiwa kuingia mjini Lubumbashi kujiunga rasmi na wababe hao wa Jamhuri ya Demokrasia Congo  siku Jumatano ya tarehe 29 mwezi January.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/37z73ar
via
logoblog

Thanks for reading TP MAZEMBE YAMREJESHA KUNDINI THOMAS ULIMWENGU KWA KANDARASI YA MIAKA MIWILI

Previous
« Prev Post