DOWNLOAD APP YETU HAPA

THE SKY MOTEL BUKOBA, KIWANJA CHA KUPUMZIKA NA KUPANGA MIPANGO YAKO.

  Masama Blog      
Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV

Katika maisha ya kawaida Kuna vitu huwezi kuvikwepa, yawezekana ukapishana navyo tu Kwa muda lakini kutokana na mazingira utakutana navyo pale inapobidi. Na hivyo ndivyo ilivyo kwa wale mnaopenda kutoka (Outing) basi hii itakuwa habari njema kwako.

Umefika Bukoba Manispaa Kwa mara ya kwanza, unahitaji kupumzika wakati ukipanga mipango yako ya kawaida, basi naomba nikuchagulie eneo maridhawa ambalo utaweza kukaa na kufurahia uwepo wako mahala pale.

The Sky Motel ni kiwanja maarufu sana kwa wakazi wa Bukoba Manispaa, kiwanja hiki kipo katikati ya Manispaa Barabara ya Uganda, hapa ndipo sehemu ambayo utapa mapumziko mazuri katika bustani nzuri ukipunga upepo mwanana, Burudani ya Muziki mwororo, vinywaji, michomo ya jikoni, huduma safi ya malazi huku usalama ukiwa ni wakutosha kwako na Mali zako.

Wapenzi wa Mpira zipo TV kubwa za ukumbini eneo la wazi, na vyumbani pia kwa huduma bora ya DSTV huku ukifurahia huduma ya mtandao (Wi-Fi Internet).

Pichani ni muonekano wa Vyumba vya kulala vyenye kila kitu ndani huduma ya mawasiliano, TV, simu, Internet, Maji ya Baridi kwa moto, vitanda venye hadhi n.k
Pichani linaonekana Jenereta maalumu (standby generator) kwa ajili ya kuhakikisha wageni mnaofika hapo hamkosi huduma ya Umeme.

Pichani ni baadhi ya michomo na mchemsho kutoka jikoni Sky Motel pamoja na michomo hiyo pia kinapikwa chakula cha haraka kulingana na mahitaji yako.

Pichani eneo la wazi la bustani ambalo linaweza kubeba watu 400 kwa wakati mmoja, sehemu ambayo pia inatumika kwa hafla mbalimbali.

Pichani Muonekano wa Jengo la The Sky Motel kama linavyoonekana upande wa mbele sehemu ya kuingilia.
Pichani kizimia Moto pamoja kamera kuhakikisha ulinzi na usalama wako na Mali zako vinazingatiwa.

Pichani Muonekano wa kaunta za Sky Motel zikiwa zimesheheni vinywaji vya aina mbalimbali.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2sMM84F
via
logoblog

Thanks for reading THE SKY MOTEL BUKOBA, KIWANJA CHA KUPUMZIKA NA KUPANGA MIPANGO YAKO.

Previous
« Prev Post