TCRA YATOA MAFUNZO KWA WATAALAMU WA TEHAMA, KUZUIA MATUKIO YA KIMTANDAO

  Masama Blog      
  Mkurugenzi wa Tehama wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Connie Francis, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati wa kufungua mafunzo ya wataalam wa tehama hapa nchini ili kuwajengea uwezo wa masula ya kimtandao.

Baadhi ya wanafunzi na wataalamu wa Tahama, wazingumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Wamesema kuwa mafunzo ya tehama ya yanayotolewa yawe na mwendelezo wake ili kudhibiti kabisa matukio ya kimtandao.
Warikili wa semina ya Tehama wakimsikiliza mtoa mada.

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inatarajia kubadilisha na kuwaongezea ujuzi wa usalama wa masuala ya Tehama wataaalam wa Tehama wa taasisi zinazotoa huduma ya intanenti nchini ili kupunguza makosa ya kimtandao ambayo hutokea.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Tehama wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Connie Francis wakati wa kufungua mafunzo ya wataalamu wa tehama wa kampuni mbalimbali zinazotoa huduma za intaneti hapa nchini jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu(BOT). Amesema mafunzo hayo yatawawezesha kuweka mifumo ya tovuti kwa usalama zaidi, kuhakikisha taarifa zinazokuwepo katika tovuti ni za uhakika na usalama.

Connie amesema kuwa kabla ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuwapa taarifa za matukio ya kimtandao, wataalamu hao wa tehama lazima wawe wameshajua viashiria vya matukio, kwani matukio haya hayatokei Tanzania Peke yake Matukio haya yanatokea dunia nzima.

Hata hivyo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) itaendelea kuwafua, watoa huduma za intaneti, na wataalamu wa tehema wa taasisi mbalimbali pamoja na wanafunzi wanaosoma masuala ya tehama hapa nchini ili kuhakikisa mapungufu ya kimtandao yanakabiliwa kabla ya kuonyesha tatizo.

Amesema katika semina hiyo watajifunza aina mbalimbali za matukio ya usalama mtandaoni, watajifunza nyezo na vitendea kazi ambavyo vitapatikana bure kabisa vitaweza kuwasaidi katika kuimarisha mifumo ya tehama.

Amesema kuwa watawapeleka katika matukio ambayo yatawasaidia kuchukua hatua kwa hatua kwa vitendo na si kinadhalia.

"Tumeweka mifumo ambayo watatumia na watajifunza kwa vitendo sasa ambapo shambulio likija wataweza kukailiana nalo, tumewaleta hapa leo ili kuweza kutupa uhakika ya mifumo, ili iweze kutegemewa na kuhakikisha kwamba uchumi wa nchini hauyumbi.

Connie ameseainisha matukio ya kimtandao kuwa ni Tovuti, (Didos Attack) matukio ya kushambulia huduma flani isipatikane,na sambulio jingine linajulikana kama fishing attack yaani ni matukio ambayo yanajiweka kama taarifa sahihi mfano barua pepe ambazo ndani kunakuwa na virusi ambavyo vinakupelekea kutuma taarifa zako sahihi na zinafanya mifumo ya kifaa cha mawasiliano kinashindwa kufanya kazi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/3aLOrGf
via
logoblog

Thanks for reading TCRA YATOA MAFUNZO KWA WATAALAMU WA TEHAMA, KUZUIA MATUKIO YA KIMTANDAO

Previous
« Prev Post