TBS YAKUTANA NA KUZUNGUMZA WAZALISHAJI,WASINDIKAJI WA BIDHAA.

  Masama Blog      
Na Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Shirika la Viwango Tanzania wanaendelea na utaratibu wao wa kutoa elimu kwa njia ya Semina katika Mikoa mbalimbali Kanda ya Ziwa, lengo likiwa ni kuwaelimisha wajasiliamali na wafanyabiashara namna bora ya kuongeza thamani ya Bidhaa zao ikiwa ni pamoja na kupata alama ya ubora.

Akizungumza baada ya semina hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora Ndg. Hamisi Sudi amesema semina hiyo inalenga zaidi kutoa Elimu juu ya viwango na udhibiti wa ubora, taratibu za kufuata ili kupata alama ya ubora, lengo ikiwa ni pamoja na kuziongezea thamani bidhaa.

Aidha Ndg. Hamisi ameongeza kuwa Semina hiyo ni sehemu ya mafunzo juu ya usajili wa bidhaa za chakula na Vipodozi ambayo ni majukumu mapya ya Shirika hilo ambapo awali yalikuwa ni majukumu ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)

Awali akifungua Semina hiyo Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Kagera Brig. Jen Marco Gaguti katika salaamu zake amewakumbusha walengwa wa semina hiyo juu ya Kuendelea kuimarisha biashara zao Kwa kuongeza thamani ya bidhaa zao, na akisisitiza kuwa Mkoa wa Kagera umepakana na Nchi Nne, hivyo Kagera ni Lango la Masoko, hivyo kama wafanyabiashara hao watatambua nafasi hiyo, inaweza kuwa chachu ya kuuza bidhaa zao Kimataifa na angetamani kuona Mkoa unafunika kwa masoko bora ukanda wa Kaskazini Magharibi.

Bi Agatha Justus ni msindikaji wa Unga wa lishe kutoka Maruku Bukoba, anasema semina hiyo imemfumbua macho na kujifunza mengi kutokana na tayari alishaanza kufanya biashara hiyo, na sasa anaanza taratibu za kupata alama ya Ubora ili bidhaa yake iweze kuuzika Kimataifa zaidi Mara baada ya kuhakikiwa na kupewa alama ya Ubora, huku akiahidi kuwa balozi wa wengine. Semina hiyo inaendelea tena Mkoani Geita, Baada ya kumaliza Kagera, na kisha wataelekea Bariadi katika kuendelea kutoa semina hiyo ya mafunzo.

 Pichani Ni Bi. Agatha Justus, msindikaji wa Unga wa lishe mshiriki wa semina na  Mjasiliamali kutoka Wilaya ya Bukoba, akionesha bidhaa yake ikiwa katika kifungashio lakini haijapewa alama ya Ubora utaratibu ukiwa tayari umeanza baada ya Semina hiyo.
  Pichani ni Wanaonekana baadhi ya Wajasiliamali wadogo wakiwa wamebeba bidhaa zao katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi, wakati wa Semina ya mafunzo kwa Wasindikaji na Wazalishaji wa Bidhaa Mkoani Kagera.
 Pichani ni Ndg. Evarist Mrema, Kaimu Mkuu wa Kanda kutoka Shirika la Viwango Tanzania, (aliesimama) akifafanua jambo wakati wa semina ya mafunzo Bukoba Manispaa Mkoani Kagera
 Pichani ni Ndg. Hamisi Sudi Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania, akitoa Hotuba kwa wadau wa semina (hawapo pichani) katika Ukumbi Wa Halmashauri Bukoba Manispaa, Mkoani Kagera.
 Pichani ni mwezeshaji kutokea Shirika la Viwango Tanzania , Bi. Fatuma akiwa anawasilisha mada wakati wa Semina ya Mafunzo Bukoba Manispaa Mkoani Kagera.
 Picha ya pamoja ya baadhi ya washiriki wa semina na Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brig. Jenerali Marco Gaguti, wakati wa semina ya mafunzo Kwa wazalishaji na wasindikaji Mkoani Kagera.from MICHUZI BLOG https://ift.tt/30DC5eA
via
logoblog

Thanks for reading TBS YAKUTANA NA KUZUNGUMZA WAZALISHAJI,WASINDIKAJI WA BIDHAA.

Previous
« Prev Post