TANESCO YAANIKA MKAKATI WA KUTATUA CHANGAMOTO YA KUKATIKA UMEME KIGAMBONI,WATOA ELIMU KWA WANANCHI

  Masama Blog      
Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii

SHIRIKA la umeme Tanzania (Tanesco) limewema limejipanga na kuweka mikakati wa kuhakikisha inaendelea kutatua changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara katika Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Moja ya mkakati huo ni kuendelea kuboresha miundombinu ya shirika hilo ikiwemo mradi wa Kituo cha kupoza umeme katika Wilaya ya Kigamboni ambao utagharimu Sh.bilioni 26 hadi utakapokamilika na mkakati huo unalenga kumaliza changamoto za kukatika kwa umeme wilayani humo.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kutoa elimu kwa wateja wa Tanesco wilayani humo Emmanuel Kezakubi aliyemwakilisha Meneja Mwandamizi wa Tanesco Kanda ya Dar es Salaam na Pwani ambapo mbali ya utoaji huo wa elimu ameeleza namna ambavyo wamejipanga kutatua changamoto ya kukatika kwa umeme.

"Kwa Wilaya ya Kigamboni Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Tanesco imedhamiria kutatua changamoto ambazo ziko kweye utoaji wahuduma kwa wateja wetu.Hivyo kuna miradi inayoendelea ukiwemo huo wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme wa kilovati 132 wilayani humo,"amesema na kuongeza kwa mipango iliyopo tatizo la kukatika umeme mara kwa mara linakwenda kupata ufumbuzi wa kudumu.

Kuhusu utoaji wa elimu,Kezakubi amesema "leo tuko Kigamboni kwa ajili ya kukutana a wateja wetu, tutaoa huduma na kusikiliza changamoto zao.Dhamira yetu ni kuwasikia wateja wetu nini ambacho wanahitaji sisi tufanye kuendelea kuboresha huduma.Ni mkutano ambao umeleta tija kubwa kwetu maana tumewasikia wateja wetu na yale ambayo yanahitaji ufumbuzi wa haraka tumeyatatua."

Pia amesema kupitia mkutano huo wametoa elimu kuhusu utunzaji wa miundombinu ya umeme pamoja na kuelezea umuhimu wa kutopanda miti katika njia ambazo umeme unapita.Kuhusu changamoto ya umeme kuwa mdogo, hiyo inaendelea kupata ufumbuzi wake kwa kujengwa kituo cha kupoza umeme.

Kwa upande wake Meneja wa Tanesco Wilaya ya Temeke Magoti Mtani amesema lengo la kutoa elimu kwa wananchi ni kuhakikisha wanakuwa na matumizi sahihi ya umeme.Pia kupokea maoni na malalamiko yao ili yafanyiwe kazi.

"Wakati mwingine wananchi wanashindwa kupeleka malalamiko yao Tanesco moja kwa moja, hivyo tumeamua kuwafuata huku huku ili kuzungumza nao.Kutoajua huduma zetu wakati mwingine inasababisha wananchi kujikuta wakiwa kwenye mikono ya vishoka,"amesema.
Pia amesema Kigamboni ina eneo kubwa la utoaji huduma kwani wanahudumia hadi eneo la Pemba Mnazi ambalo ni zaidi ya kilometa 80 kutoka Kituo kilipo. Kuhusu walikotoka na walipo , Mhandisi Mtani amesema kwa sasa mambo yanakwenda vizuri na malalamiko yameendelea kupungua.
  Kazi ya utoaji elimu na kushughulikia matatizo kwa baadhi ya wateja wa Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco) ikiendelea kutolewa na maofisa wa shirika hilo kwa wananchi wa Wilaya ya Kigamboni.
 Ofisa Habari Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilayani Temeke akitoa elimu ya uokoaji wakati wa mkutano huo.
 Ofisa Huduma kwa Wateja wa Tanesco -Temeke jijini Dar es Salaam Chacha Ndege(kushoto) akifafanua jambo kwa wateja waliofika kwenye meza yake wakati wa mkutano wa utoaji elimu kwa wateja.
 Meneja wa Wilaya wa Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco) Mhandisi Magoti Mtani (kulia)akizungumza na baadhi ya wateja wa shirika hilo Wilaya ya Kigamboni wakati wa mkutano wa kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya umeme na kupokea kero za wateja
wakati wa shirika hilo.
 Muuguzi kutoka Shirika la Umeme Tanzania Neema Kombo(kushoto) akitoa huduma ya vipimo kwa moja ya wateja wakati wa mkutano huo wa utoaji elimu kwa wateja.
 Maofisa wa Tanesco wakijadiliana jambo wakati wa mkutano wa utoaji wa elimu kuhusu nishati ya umeme, kupokea malalamiko na utoaji huduma kwa wateja uliofanyika wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.


Mwakilishi wa Meneja Mwandamizi wa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Tanesco Emmanuel Kezakubi(wa pili kushoto) akifuatilia kwa makini mkutano wa utoaji elimu kwa wananchi ulioandaliwa na shirika hilo.
 Ofisa Huduma kwa Wateja wa Tanesco Chacha Ndege(katikati) akitoa huduma kwa mmoja ya wateja wa Tanesco wilayani Kigamboni.
 Ofisa wa Tanesco(kulia) akitoa elimu ya matumizi sahihi ya umeme wa majumbani kwa wanafunzi ambao walifika katika mkutano uliondaliwa na Tanesco kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi na kupokea kero mbalimbali na kisha kuzipatia ufumbuzi wake.
 Mmoja ya wakazi wa Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam (kushoto)akitoa maelezo kwa watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco) baada ya shirika hilo kwenda kutoa elimu na kupokea maoni kwa wateja wao wa wilaya hiyo.from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2U3thxp
via
logoblog

Thanks for reading TANESCO YAANIKA MKAKATI WA KUTATUA CHANGAMOTO YA KUKATIKA UMEME KIGAMBONI,WATOA ELIMU KWA WANANCHI

Previous
« Prev Post