DOWNLOAD APP YETU HAPA

Taifa Stars yaangukia kundi J kusaka tiketi ya Kombe la Dunia 2022

  Masama Blog      
Na Yassir Simba, Globu ya Jamii

Timu ya taifa, Taifa Stars imeangukia kundi J katika hatua za awali kusaka tiketi ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia 2022 yatakayofanyika huko nchini Qatar.

Mashindano hayo yatakuwa na jumla ya makundi 10 ambayo yatacheza hatua za awali kabla ya kupata timu 5 zitakazo wakilisha bara la Afrika katika fainali hizo za kombe la dunia.

Tanzania imeangukia kundi J sambamba na timu nyengine tatu ambazo ni Congo DRC, Benin na Madagascar. Mechi 120 za awali zinatarajiwa kuanza kupigwa kabla ya mechi 10 ambazo ni za mtoano ili kupata timu 5 ambazo zitawakilisha bara la Afrika katika kombe la Dunia mwaka 2022.

Kundi linalotajwa kuwa ni kundi gumu zaidi ni kundi G lenye timu za Ghana, South Africa, Zimbabwe na Ethiopia.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36glIG3
via
logoblog

Thanks for reading Taifa Stars yaangukia kundi J kusaka tiketi ya Kombe la Dunia 2022

Previous
« Prev Post