TAEC YATOA ELIMU CHUO CHA SAUTI KAMPASI YA MALIMBE JUU YA MATUMIZI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA

  Masama Blog      
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu ya Atomiki Nchini  (TAEC )Nchini Profesa Lazaro Busagala 
Dr. Remigius Kawala, Mtafiti na Mratibu wa Tafiti na Mafunzo wa Tume ya Nguvu za Atomiki Nchini(TAEC)
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sauti kilichopo Jijini Mwanza wakuwa katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na TAEC
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sauti kilichopo Jijini Mwanza wakuwa katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na TAEC
 Mafunzo yakiendelea kama inavyoonekana katika picha katika Chuo Kikuu cha Sauti Kilichopo Jijini Mwanza
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sauti kilichopo Jijini Mwanza wakuwa katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na TAEC


Na.Vero Ignatus

Tume ya nguvu za Atomiki nchini imeendesha semina na kutoa  Elimu juu ya matumizi ya Sayansi ya Teknolojia ya Nyuklia katika Maktaba ya chuo cha Mtakatifu Augustino (Sauti) Kampasi ya Malimbe

Mkurugenzi Mkuu wa TAEC nchini Profesa Lazaro Busagala alisema jukumu la  Tume  hiyo ni Kusimamia na kudhibiti matumizi salama ya mionzi ili kulinda umma, wafanyakazi pamoja na mazingira dhidi ya madhara ya mionzi na kuhamasisha matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia kwa maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.

Prof.Busagala alisema Elimu hiyo ni muhimu katika sekta ya Afya Kilimo,mifugo,Viwanda,maji,ujenzi, pamoja na Kufanya utafiti na kutoa ushauri na taarifa mbali mbali juu ya Sayansi na Teknolojia ya Nyukilia

Awali  Dr. Remigius Kawala, Mtafiti na Mratibu wa Tafiti na Mafunzo TAEC alisema mafunzo hayo yamejumuisha Wakufunzi,watafiti,wafanyakazi,wanafunzi ili kuwajengea uwezo juu ya udhibiti  wa mionzi na uhamasishaji na uendelezaji wa matumizi salama ya Teknolojia ya Nyuklia katika sekta mbalimbali .

Aidha mkutano huo ulilenga kuwaleta watafiti pamoja ili kubadilishana uzoefu kwenye nyanja ya Sayansi na Teknolojia sambamba na matumizi salama ya Teknilojia ya nyuklia mahaka pa kazi na jamii kwa ujumla.

Dkt.Kawala alisema kuwa Mafunzo hayo ni endelevu ambapo januari 28-2020 watakuwa Visiwani Zanzibar katika State University of Zanzibar  (SUZA).

Amesema mafunzo hayo ni moja ya maandalizi ya mkutano wa maonyesho wa Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia unaotegemewa kufanyika tarehe 3-5 mwaka 2020 Jijini Arusha

Ifahamike kuwa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na.7 yamwaka 2003 (The Atomic Energy Act. No.7 of 2003). Awali ilikuwa ikijulikana kama Tume ya Taifa ya Mionzi (National Radiation Commission) iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Na.5 ya mwaka 1983 (The Protection from Radiation Act. No.5 of 1983)

Kulinga na na kifungu Na.6(1) cha Sheria ya Nguvu za Atomiki. Majukumu ya TUME ni Kudhibiti matumizi salama ya mionzi nchini,Kuhamasisha na kupanua matumizi salama ya Teknolojia ya Nyuklia.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2uI7pgg
via
logoblog

Thanks for reading TAEC YATOA ELIMU CHUO CHA SAUTI KAMPASI YA MALIMBE JUU YA MATUMIZI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA

Previous
« Prev Post