TAASISI YA AMANI TANZANIA ,VIONGOZI WA DINI WAUNGA MKONO KAULI YA RAIS MAGUFULI... WAHIMIZA WATANZANIA KUAMINIANA, KUPENDANA

  Masama Blog      

Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

TAASISI ya Amani Tanzania (TIPF) kwa kushirikiana na viongozi wa dini hiyo wameunga mkono Kauli ya Ris Dk.John Magufuli kuhusu tabia ya baadhi ya watu kueleza kila mtu asiyepatikana katika maeneo anayoishi kuwa ametekwa na kwamba huko ni chanzo cha kutokuaminiana katika jamii ya Watanzania na hivyo kupoteza amani.

Akizungumza leo Januari 15 mwaka 2020 jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi ya Amani Tanzania(TIPF) Sadiki Godigodi amesema kuwa amesema vitendo hivyo vya uzushi havijengi umoja bali vinatengeneza dhana hasi miongoni mwa watanzania.

Amesema kuwa wameamua kuunga mkono kauli ya Rais Magufuli aliyotoa akiwa katika ziara yake visiwani Zanzibar kuhusu watu wenye tabia ya kuvinyooshea vidole vyombo vya ulinzi na usalama na kwamba wao wanasema kuwa Wwatanzania lazima  wawe makini na kauli wanazotoa kutokana na mambo yanayotokea nchini.

"Tulizaliwa Tanzania na tutazikwa Tanzania,vizazi vyetu vitatuhukumu kwa mambo tunayofanya sasa ambayo kimsingi yataathiri maisha ya baadaye.Tunakemea  vitendo vya kunyooshea vidole vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuwa wajibu wa vyombo hivyo kuhusu usalama wa nchi  kwani bila wao amani haipo ,huku vikiwa na heshima kubwa ndani nan je ya nchi hivyo ni vema kuheshimika,"amesema.

Kwa upande wake Sheikh wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Mohamed Muyenga amesema wanoafanya vitendo hivyo wanatenda dhambi  na kwamba waliopata matatizo taarifa zao ziko katika vyombo husika kwa ajili ya hatua mbalimbali za kushughulikia matatizo hayo.

Hata hivyo amesema wanatoa pongezi kwa Rais kwa upendo wake kwa wananchi pamoja na kutanguliza maslahi mapana kwa nchi yetu na kubwa zaidi kila Mtanzania ni vema akafahamu kuwa ni jukumu letu sote kuhakikisha nchi inakuwa salama.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Amani Tanzania(TIPF) Sadiki Godigodi katikati akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu kuunga mkono kauli ya Rais Dk.John Magufuli
Mwenyekiti wa Taasisi ya Amani Tanzania Sadiki Godigodi(kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2tZrXRe
via
logoblog

Thanks for reading TAASISI YA AMANI TANZANIA ,VIONGOZI WA DINI WAUNGA MKONO KAULI YA RAIS MAGUFULI... WAHIMIZA WATANZANIA KUAMINIANA, KUPENDANA

Previous
« Prev Post