SPIKA NDUGAI AWAKABIDHI MASPIKA WASTAAFU MAJOHO YAO BUNGENI JIJINI DODOMA

  Masama Blog       Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akimvalisha na kumkabidhi joho Mhe. Pius Msekwa alilokuwa akitumia wakati akiwa Spika wa Bunge la Nane Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai.
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Wabunge nje ya ukumbi wa Bunge baada ya wa Sherehe fupi za kukabidhiana majoho kwa Maspika wastaafu zilizofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma. Kuanzia kulia waliokaa ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Spika Mstaafu, Mhe. Anne Makinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, Spika Mstaafu, Mhe. Pius Msekwa, Mbunge wa Urambo Mhe. Margaret Sitta na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) katika picha ya pamoja na Maspika wastaafu ambao ni Mhe. Anne Makinda (wa pili kushoto) na Mhe. Pius Msekwa (wa pili kulia) baada ya Sherehe fupi za kukabidhiana majoho kwa Maspika hao zilizofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na Mbunge wa Urambo, Mhe. Margaret Sitta.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akimkabidhi joho Mhe. Margaret Sitta kwa niaba ya mume wake aliyekuwa Spika wa Bunge la 9 Mhe. Samuel Sitta wakati wa Sherehe fupi za kukabidhiana majoho kwa Maspika wastaafu zilizofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akimpa mkono wa pongezi Spika wa Bunge la Kumi Mhe. Anne Makinda baada ya kumkabidhi joho alilokuwa akitumia wakati akiwa Spika wa Bunge la Kumi.PICHA NA BUNGE


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/37BXE1Y
via
logoblog

Thanks for reading SPIKA NDUGAI AWAKABIDHI MASPIKA WASTAAFU MAJOHO YAO BUNGENI JIJINI DODOMA

Previous
« Prev Post