DOWNLOAD APP YETU HAPA

SimbaNET yapata Mkurugenzi mpya

  Masama Blog      
Kampuni ya Wananchi Group imemteua Kennedy Ojung'a kuwa Mkurugenzi Mkuu wa SimbaNET.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam,
Kennedy atawajibika kwenye mipango ya biashara na ukuaji wa SimbaNET katika mikoa na maeneo ya nchi mbalimbali ambayo biashara inafanyika ikiwamo Tanzania.
Taarifa hiyo imeeleza pia kuwa Kennedy anachukua jukumu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa zamani aliyeachishwa kwa madai ya udanganyifu.
SimbaNET hutoa huduma mbalimbali ikiwemo uunganishwaji, usanifu, usalama na huduma zinazosaidia biashara ili kuboresha mazingira yao ya habari na teknolojia ya mawasiliano (ICT).
SimbaNET ni kampuni tanzu ya Mwananchi Group ambayo hutoa huduma nchi mbalimbali kama Kenya, Tanzania, Uganda, Zambia, Malawi na UAE. Pia hutoa huduma katika nchi zingine kama vile Rwanda, Burundi, SA, Msumbiji, Nigeria, Ghana, Sudani Kusini, DRC kupitia washirika wao.
Orodha ya wateja wa kampuni hiyo inajumuisha benki kadhaa kubwa za Afrika Mashariki, mahoteli, kampuni za bima, Taasisi za elimu na Taasisi na Wakala. Lengo la msingi la kampuni hiyo ni kutoa huduma za juu zaidi na kwa wakati, zilizodhibitiwa kwa kufuata Mikataba ya Kiwango cha Huduma (SLAs).


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2RjaLOD
via
logoblog

Thanks for reading SimbaNET yapata Mkurugenzi mpya

Previous
« Prev Post