Ticker

10/recent/ticker-posts

SHAMBA LA MITI SAOHILI WAKABIDHI MADAWATI KWA SHULE YA MSINGI MBALWE WILAYANI MUFINDI


Na Ripota Wetu,Michuzi Globu ya jamii

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) kupitia Shamba la Miti SaoHill limekabidhi madawati katika Shule ya Msingi Mbalwe iliyopo katika Kijiji cha Wami Mbalwe Wilayani Mufindi.

Madawati hayo yamekabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. David Willium kwa niaba ya Shule hiyo ikiwa ni sehemu ya kuchangia shughuli za maendeleo katika vijiji vinavyolizunguka shamba.

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa madawati hayo Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William amesema anaipongeza TFS kupitia Shamba la Miti SaoHill kwa jitihada wanazozionesha  kwa kushirikiana na jamii kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo Wilayani.

“Nawapongeza sana SaoHill kwa kuwa majirani wazuri wa wananchi, mmetuchangia madawati 30 lakini bado tuna mahitaji ya madawati sehemu nyingine endeleeni kutusaidia,” amesema William

Ameongeza kuwa anatoa mwito kwa wadau wengine wilayani kuendelea kuchangia shughuli za maendeleo na hivyo viongozi katika maeneo husika kuhakikisha wanasimamia vyema maendeleo hayo.

Aidha Kaimu Meneja wa Shamba la Miti SaoHill Daniel Silima amesema ugawaji wa madawati haya 30 ni sehemu tu ya jitihada za kuonyesha ushirikiano katika jamii inayolizunguka shamba.

 Silima amesema hiyo ni sehemu ya kurejesha fadhira kwa jamii ambayo inazunguka shamba kwani wamekuwa ni sehemu kubwa katika ulinzi wa misitu katika Wilaya ya hiyo ya Mufindi.

Hadi sasa TFS kupitia Shamba la Miti SaoHill limetoa madawati zaidi ya 1,000 katika jamii inayolizunguka shamba ikiwa ni pamoja na nje ya Wilaya ya Mufindi.
Pichani:Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe.Jamhuri William akikabidhiwa madawati na Kaimu Meneja wa Shamba la Miti SaoHill Bw.Daniel Silima katika makabidhiano ambayo yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Mbalwe



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2u0oGBm
via

Post a Comment

0 Comments