SERIKALI YAANDAA MKAKATI WA MIAKA MITANO WA KUKUZA ZAO LA PAMBA

  Masama Blog      

Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imesema imetengeneza mkakati wa miaka mitano kuhusu sekta ndogo ya pamba ili kukidhi mahitaji ya soko na upatikanaji wa pembejeo kwa wakulima nchini.

Kauli hiyo Imetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Hussein Bashe wakati akifungua mkutano wa kamati ndogo ya wadau wa kilimo iliyokutana jijini Dodoma.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Wakuu wa mikoa inayolima zao la pamba nchini ambao wamepokea na kujadili taarifa ya kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza changamoto zinazoikabili tasnia na kutoa mapendekezo ya utatuzi wake.

Kamati ndogo ya wadau iliundwa Octoba mwaka jana jijini Mwanza kwa lengo la kuja na mapendekezo ya utatuzi wa changamoto za zao hilo nchini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mh Bashe amesema kikao hicho ni uhimu ili kutengeneza mustakabali mzuri wa tasnia ya pamba kwenye mikoa 17 inayolima zao hilo.

Bashe amesema msimu ujao wa kilimo cha pamba unapaswa uwe mzuri na usiwe na matatizo licha ya mikao michache bado kuwa na takribani asilimia 20 ya pamba isiyonunuliwa hadi sasa.

“Pamba na kilimo ni biashara tusipeleke siasa.Msimu huu ulikuwa mgumu. Tumekubaliana serikalini kuwa biashara hii ifanywe kwa uwazi zaidi ili mkulima apate manufaa ya jasho lake” amesema Bashe.

Bashe amesema tayari wizara ya Kilimo imefanya majadiliano na wizara za Viwanda na Biashara na ile ya Fedha na Mipango  juu ya mustakabali wa zao hilo msimu ujao.

“ Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya  2015-2020 imeelekeza ushirika kusimamia sekta ya pamba kwa manufaa ya wakulima nchini,hivyo lazima tutafute suluhu ya changamoto za masoko “ Amesema Bashe.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya wadau wa pamba  Adamu Malima  amesema ni wakati wa wizara ya kilimo kuweka mikakati mahsusi ya upatikanaji wa bei nzuri ya pamba ya wakulima kupitia mfumo wa ushirika.

“Ushirika nchini lazima uwe na takwimu sahihi za wakulima,kiasi cha pembejeo kinachotakiwa na eneo linalolimwa ili kuepusha hasara kwa wakulima kubebeshwa madeni yasiyo wahusu” Amesema Malima.

RC Malima amebainisha kuwa suala la utafiti  na ugani kwenye zao la pamba ni muhimu lipewe kipaumbele lakini   wizara ya kilimo haioneshi jitihada.

Amesema Wizara ya Kilimo inatakiwa pia kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo za pamba kwa wakati na zenye ubora  kuhakikisha zinawafikia kwa wakati na bei nafuu.

Kikao hiko maalum cha wadau wa Pamba kimehudhuriwa na Wakuu wa Mikoa ya Mara, Simiyu, Morogoro, Kagera,Kigoma, Singida, Mwanza, Geita, Shinyanga, Kilimanjaro na  Katavi.
 Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Hussein Bashe akizungumza na Wakuu wa Mikoa inayolima Pamba Katika mkutano wa kujadili zao hilo uliofanyika jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akizungumza na Wakuu wa Mikoa inayolima Pamba sambamba na wadau wa zao hilo wakati akifungua mkutano wa pamoja wa kujadili maendeleo ya zao hilo linalolimwa takribani Mikoa 17 nchini. Mkutano huo umefanyika jijini Dodoma.
 Baadhi ya Wakuu wa Mikoa inayolima Pamba wakifuatilia mkutano wa pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Hussein Bashe na wadau wa zao hilo jijini Dodoma.
 Wadau mbalimbali wa zao la Pamba wakifuatilia mkutano wao wa pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Hussein Bashe na Wakuu wa Mikoa inayolima zao hilo.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe Rehema Nchimbi akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa wenzake wanaolima Pamba Katika mkutano wa kujadili maendeleo ya zao hilo uliofanyika jijini Dodoma na kuhudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Hussein Bashe.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/38ESzG7
via
logoblog

Thanks for reading SERIKALI YAANDAA MKAKATI WA MIAKA MITANO WA KUKUZA ZAO LA PAMBA

Previous
« Prev Post