SAYONA DRINKS LIMITED YAINGIZA KINYWAJI CHA ‘ TWIST’ SOKONI,HARMONIZE AWA BALOZI WAKE

  Masama Blog      

Balozi wa Kinywaji cha Sayona Twist, Rajabu Abdul Kahali almaarufu, Harmonize akinywa kinywaji kipya cha Sayona Twist wakati wa hafla ya uzinduzi uliofanyika Januari 15,2020 jijini Dar es salaam. Pamoja nae kushoto ni viongozi kutoka Motisun Group.

Balozi wa Kinywaji cha SayonaTwist, Rajabu Abdul Kahali almaarufu, Harmonize akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji cha Sayona Twist uliofanyika Januari 15,2020 jijini Dar es salaam. Pamoja nae kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya Motisun Group, Subhash Patel na wengine ni viongozi kutoka Sayona Group.
Balozi wa Kinywaji cha Sayona Twist, Rajabu Abdul Kahali almaarufu, Harmonize akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji cha Sayona Twist uliofanyika  Januari 15,2020 jijini Dar es salaam. Pamoja nae kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Motisun Group Veer Patel, Mwenyekiti wa bodi ya Motisun Group, Subhash Patel, Mkurugenzi Mtendaji wa Sayona Drinks Limited, Pawan Patel, Mkurugenzi Mkuu wa Sayona Group, Nitin Menon na Meneja wa Harmonize, Sebastian Ndege maarufu kama Jembe ni Jembe.

Mwenyekiti wa bodi ya Motisun Group, Suhbash Patel (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji cha Sayona Twist uliofanyika jijini Dar es salaam  Januari 15,2020. Pamoja nae kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Motisun Group Veer Patel na Balozi wa Kinywaji cha SayonaTwist, Rajabu Abdul Kahali almaarufu, Harmonize.
 
Wateja wa vinywaji vya Sayona, sasa watakuwa na fahari ya kuchagua zaidi baada ya kampuni inayotengeneza vinywaji baridi ambayo inakuwa kwa kasi jijini Dar es salaam, Sayona Drinks Limited kuboresha na kuzindua upya kinywaji kinachofahamika kwa jina la TWIST.

Kampuni ya Sayona imedhamiria kuwapa machaguo mengi zaidi wateja wake ili kukidhi hitaji za ladha mbalimbali zinazopendwa na wateja.

Akizungumza wakati wa hafla ya utambulisho wa bidhaa hiyo, Pawan Patel, Mkurugenzi Mtendaji wa Sayona Drinks Limited alisema, “Twist ni kiburudisho chenye ladha nzuri, kinachokupa thamani ya pesa yako. Twist inakuja na ladha saba za kipekee ikiwemo ya pasheni, chungwa, limao, embe, nanasi, tangawizi na ladha ya Cola,”

Pia amebainisha kuwa Kampuni itatangaza ujio wa ladha nyingine za kipekee katika siku za usoni. Aliongeza kuwa, Sayona, imedhamiria kukidhi hitaji la wateja wake ndiyo maana wameendelea kuwa wabunifu na kila mwaka wamekuwa wakitambulisha bidhaa mpya sokoni.

“Tunaamini kupitia Twist, tunayo bidhaa bora ambayo ina utofauti na bidhaa nyingine zilizopo sokoni, kuwapa wateja wetu kiburudisho chenye ladha nzuri na ya kipekee,"alisema.

Kwa upande wake, Nitin Menon, Mkurugenzi Mkuu wa Sayona Drinks Ltd Group yeye alizungumzia juu ya utoaji wao huduma kwa wateja na gharama za bidhaa hii mpya.

Menon alisema, hatua ya kuizindua Twist ni matokeo ya kazi kubwa inayofanyika ya kuimarisha ukuaji wa kampuni kupitia mkakati kabambe ambao unaenda sambamba na badiliko la ladha kwa watumiaji na tabia katika ununuzi.

“Bidhaa yetu mpya ya Twist inakuja kwa ujazo wa milimita 300 na 400 katika chupa ya plastiki. Bidhaa itauzwa kwa bei ya rejareja ya shilingi 500 na itapatikana nchi nzima,” aliongeza.

Aidha, alitumia fursa hiyo kuutangazia umma kuwa, wameingia makubaliano na staa wa bongo fleva, Rajabu Abdul Kahali (Harmonize) kuwa balozi wa heshima wa bidhaa za Sayona, ambaye pia alishiriki katika uzinduzi huo.

“Tunajisika fahari kuwa na Harmonize kama balozi wa heshima wa bidhaa yetu. Ni miongoni mwa vijana wapambanaji, mwenye msaada kwa watanzania wengi, anayefanya kazi kwa bidii, lakini pia amekuwa na chachu ya kuupeleka muziki wa Tanzania mbali zaidi. Hili ni Jambo ambalo linaunga mkono malengo na maono yetu ya kuwa kinara katika biashara ya vinywaji baridi barani Afrika,” alisema Menon.

“Tuna imani kwamba ushirikiano huu utawezesha vinywaji vya Sayona kuwa miongoni mwa bidhaa zenye nguvu zaidi Tanzania. Harmonize atatusaidia kuwafikia walengwa wetu nchini Tanzania na sisi kufanya naye kazi kama balozi, ni miongoni mwa hatua muhimu ya yeye kushiriki katika miradi yetu mingi inayokuja.”

Kwa upande wa Harmonize, alisema ni jambo la faraja kufanya kazi na Sayona Drinks Limited na huu ni mwanzo wa ushirikiano mzuri zaidi baina yake na kampuni.

Akizungumzia juu ya uzinduzi wa bidhaa hiyo, Harmonize amesema, “Twist ni kinywaji kizuri chenye ladha za kipekee. Nimekuwa nikikitumia mara kwa mara na nimekuwa sehemu ya ubunifu huu mpya wa bidhaa hii, nina hakika kuwa Watanzania watafurahia bidhaa hii na matumizi yake yatafika nje ya Tanzania. Pia ninajisikia fahari sana kujumuishwa ndani ya Sayona Group ambao wamekuwa na sifa kubwa ya ubora wa bidhaa zao,” alimalizia.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2TuRAUM
via
logoblog

Thanks for reading SAYONA DRINKS LIMITED YAINGIZA KINYWAJI CHA ‘ TWIST’ SOKONI,HARMONIZE AWA BALOZI WAKE

Previous
« Prev Post