RC MAKONDA AZINDUA MFUMO WA KURATIBU NA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO KIDIGITALI.

  Masama Blog      
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amezindua mfumo wa kuratibu na kusimamizi miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Mkoa huo kwa njia ya mtandoa kwa lengo kuongeza Chachu na kasi ya uwajibikaji kwa Viongozi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa taarifa sahihi za miradi ya maendeleo jambo litakalopunguza tatizo la miradi kusuasua.

RC Makonda amesema kwa muda mrefu baadhi ya Watendaji walikuwa wakitoa taarifa za wongo kwa viongozi kuwa mradi unaendelea vizuri na upo katika hatua nzuri lakini kiongozi anapofika kwenye eneo husika anakuta hakuna kinachoendelea lakini kupitia mfumo huo kiongozi ataona kila kitu kinachoendelea kwenye mradi kwa kutumia Computer au Simu ya mkononi.

Aidha RC Makonda amesema ndani ya mfumo huo zitapatikana taarifa zote muhimu za miradi ikiwemo Msimamizi wa Mradi, Mkandarasi, Gharama za mradi, Muda wa mradi kukamilika, fedha iliyolipwa, hatua mradi ulipofikia pamoja na Mamlaka ya serikali ya mtaa ambapo mradi husika unatekelezwa.

RC Makonda amesema faida za mfumo ni pamoja kuongeza Uwazi, uwajibikaji wenye tija.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2RjGsr2
via
logoblog

Thanks for reading RC MAKONDA AZINDUA MFUMO WA KURATIBU NA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO KIDIGITALI.

Previous
« Prev Post