Rais wa China atoa angalizo dhidi ya virusi vya corona

  Masama Blog      
 Mlipuko wa virusi vipya vinavyouwa vinasambaa kwa kasi, Rais Xi Jinping ametoa tahadhari baada ya kufanya kikao maalum katika siku ya mwaka mpya wa Lunar.

Rais aliwaambia maofisa wa ngazi za juu kuwa nchi iko kwenye hali ya hatari kubwa , kwa mujibu wa televisheni ya taifa.Virusi vya corona tayari vimeuwa watu wapatao 41 na wengine 1,400 wameambukizwa tangu virusi hivyo vigundulike huko Wuhan.

Tayari miji mingi imeweka katazo la kusafiri kwa watu wake.
Na siku ya jumapili hata magari binafsi hayataruhusiwa kutoka Wuhan, eneo ambalo virusi hivyo viibainika kwa kwa mara ya kwanza.

Hospitali nyingine ya dharura inajengwa na inategemewa kuwa ndani ya wiki , itaweza kuwahudumia wagonjwa wapya 1,300, na itamalizika kujengwa ndani ya nusu mwezi, gazeti la serikali la la People's Daily limeripoti.from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2O0GMKy
via
logoblog

Thanks for reading Rais wa China atoa angalizo dhidi ya virusi vya corona

Previous
« Prev Post