PWANI - MOROGORO USAJILI WA WATOTO WAVUNJA REKODI

  Masama Blog      
Wakazi wa Mikoa ya Morogoro na Pwani wameendelea kujitokeza na kuwasajili watoto wao walio na umri chini ya miaka mitano katika zoezi linaloendelea kwa mikoa hiyo miwili.

Katika hali isiyo ya kawaida tayari takwimu zinaonesha kufikia lengo ndani ya kipindi kifupi ukilinganisha na matarajio ya awali ya kufikisha asilimia mia moja ndani ya kipindi cha miezi mitatu, tayari Mkoa wapwani unaongoza kwa kusajili wenye watoto 179,162 na kusajili watoto wapatao 178,471 ambayo ni sawa na asilimia 99.6% kwa Mkoa wa Morogoro wenye jumla ya watoto 381,568 na kusajiliwa watoto 310,616 sawa na asilimia 81.4.

Halmashauri zinazoongoza kwa Mkoa wa Pwani ni Bagamoyo DC imesasili watoto wote 19,102, Kibaha DC watoto 11,461 Kisarawe DC watoto 18098 Mkuranga DC watoto 37,279 sawa na asilimia 100% kwa zote na kwa upande wa Morogoro Halmashauri ya Malinyi imesajili watoto wote wapatao 22,878 na kufuatiwa na Halmashauri ya Kilombero watoto 45, 528 na Halmashauri ya Mvomero DC watoto 51837 sawa na asilimia 91.4, Halmashauri zilizobaki zinaendelea vizuri kwa ujumla wake ni asilimia 80% ya watoto wamesajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa.

Mpango huo ulianza kutekelezwa rasmi katika Mikoa hiyo miwili mnamo tare 6 Desemba 2019 na kuzinduliwa Kitaifa Mkoani Morogoro tarehe 11 Desemba 2019 ambapo Waziri wa Katiba na sheria Mhe. Balozi Augustine Mahinga alikuwa mgeni rasmi huku kukihudhuriwa na taasisi mbalimbali za serikali na mashirika ya kimataifa.

Awali akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Afisa Mawasiliano wa RITA Bw Jafari Malema amesema kuwa takwimu za sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012, zinaonesha Mikoa ya Pwani na Morogoro ni miongoni mwa Mikoa yenye idadi ndogo ya wananchi waliosajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa ambapo kwa mujibu wa takwimu Mkoa wa Pwani ni asilimia 14.5 na Morogoro ni asilimia 11 pekee ya wakazi wote waliosajiliwa na kupatiwa nyaraka hiyo muhimu.

Malema ameongeza kuwa Mafanikio hayo ni muendelezo wa maboresho yaliyofanyika hasa katika upande wa teknolojia ya utumaji wa taarifa za watoto waliosajiliwa, tunatumia simu za mkononi zilizowekwa programu maalumu kuwesensha kusajili na kutuma taarifa kwa wakati, pia vituo ya usajili vimesogezwa karibu na makazi ya wananchi, usajili unafanyika katika ofisi za kata na vituo vya tiba vinavyotoa huduma ya mama na motto na mwisho tumeondoa ada ya malipo ya cheti hivyo vyeti vinapatikana bure.

‘’Mpaka sasa Mikoa kumi na mitano inatekeleza mpango huo ambayo ni Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Lindi, Mtwara, Mwanza, Geita, Shinyanga, Mara, Simiyu, Singida na Dodoma Morogoro na Pwani na kufanikiwa kusajili zaidi ya asilimia 49 kutoka asilimia 13 ya mwaka 2012’’.alisema Malema.

RITA inatekeleza mpango wa usajili na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa watoto wa umri chini ya miaka mitano mara baada ya kufanyiwa majaribio katika manispaa ya Temeke Jijini Dar es salaam mnamo mwaka 2012 kisha baadaye kuanza rasmi kutekelezwa katika Mikoa ya Mbeya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kitaifa na kimataifa kama vile Wizara ya Afya maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Shirika la kimataifa la kuhudumia watoto Duniani (UNICEF), Serikali ya Canada na Kampuni ya simu za mkononi TIGO.
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Augustine Mahiga akimkabidhi cheti cha mtoto mmoja wa wananchi waliohudhuria uzinduzi siku hiyo.
Baadhi ya wananchi wakipatiwa huduma Mkoani Morogoro.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2szdk73
via
logoblog

Thanks for reading PWANI - MOROGORO USAJILI WA WATOTO WAVUNJA REKODI

Previous
« Prev Post