Prince Harry na William wakanusha taarifa za kuvutana kwao

  Masama Blog      
Wajukuu wa Malkia nchini Uingereza William na Harry wameipuuza ripoti ya gazeti moja hii leo inayozungumzia kuwepo mvutano mkubwa katika uhusiano wao, wakisema taarifa hiyo ni ya kukera na ya uharibifu mkubwa wakati wakirejea kwenye mazungumzo kuhusiana na mustakabali wa ufalme huo wa Uingereza. 

Ndugu hao wawili walitowa taarifa isiyokuwa ya kawaida hata wakati Malkia Elizabeth wa Pili anapojiandaa kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na mwanamfalme Harry kwa mara ya kwanza tangu alipotangaza pamoja na mkewe Meghan mpango wao wenye utata wa kutaka kuyaachia majukumu ya taasisi hiyo ya kifalme. Mkutano huo wa aina yake wa kifamilia unalenga kuweka mwelekeo wa mustakabali wa wanandoa hao.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/30hgsRn
via
logoblog

Thanks for reading Prince Harry na William wakanusha taarifa za kuvutana kwao

Previous
« Prev Post