Ticker

10/recent/ticker-posts

PAMOJA NA CHANGMOTO YA UHABA WA MADARASA,ARUMERU YAZIDI KUJIPANGA KUONGEZA KIWANGO CHA UFAULU KWA WANAFUNZI

NaJusline Marco-Arumeru,Arusha
,
Kufuatia ongezeko la wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika Wilaya ya Arumeru baadhi ya shule za sekondari Wilayani humo zinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa madarasa kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi wanayoipata kuzidi uwiano wa kitaaluma.

Shule ya sekondari Ngongongare iliyopo Wilayani humo ni miongoni mwa shule zilizopokea wanafunzi wengi kuzidi uwiano wa kitaaluma jambo linalosababisha mlundikano wa wanafunzi madarasani.

Akitoa taarifa ya upokeaji kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule hiyo mkuu wa shule hiyo mwalimu Sophia Warioba amesema kuwa tayari wamepokea wanafunzi 347 ambao wanatazamiwa kuanza masomo yao ifikapo januari 16 mwaka huu kama ambavyo agizo la Waziri Mkuu linavyoelekeza.

Sophia amesema kuwa idadi hiyo ya wanafunzi katika shule anayoisimamia imekuwa changamoto kubwa kutokana na uhaba wa madarasa uliopo ambapo mpaka sasa shule hiyo ina uhaba wa madarasa 6 kwani yaliyopo ni madarasa 3 ili kufikisha idadi ya madarasa 9 ambayo yataweza kukidhi idadi hiyo ya wanafunzi kwa uwiano uliopitishwa na serikali.

Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari Momela mwalimu Hassan Rajab Ndutwe amesema kuwa shule hiyo inavyumba 10 vya madarasa ambavyo havitoshelezi mahitaji ya wanafunzi hao kutokana na ukosefu wa madarasa 4 kulingana na idadi ya wanafunzi wapya kufika 185.

Naye mwenyekiti wa halmashauri ya Meru  Wilayani humo Wille Njau amewataka wakuu wa shule hizo kutumia njia mbadala ili kuweza kuwapokea watoto wote waliochaguliwa ifikapo tarehe 16 mwezi huu huku wakiendelea na jitihada za ujenzi wa madarasa yaliyobaki kwa muda mfupi uliopo kwa kushirikiana na wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Ameongeza kuwa ni vyema viongozi wa kata husika na walimu wakuu wakajitathimini upya juu ya michango waliyoipitisha kwa wananchi wao na kuiongeza ili waweze kufikia lengo la ujenzi wa madarasa bora yenye viwango vinavyohitajika na kuondoa changamoto wa kuwaweka wanafunzi wengi mahali pamoja.

Pamoja na hayo wilaya ya Arumeru imekuja na mpango mkakati wa kuhakikisha wanaongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi katika kipindi hiki cha mwaka 2020 kwa kutengeza mfumo wa kuimarisha miundombinu ya elimu.
 Wanafunzi wa kidato cha kwanza wakijisomea huku wakisubiri masomo rasmi yaanze januari 16 mwaka huu.
 Wanafunzi wa kidato cha kwanza waliochaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari wakiwa katika darasa moja wakisubiri umaliziwaji wa madarasa yao katika shule sekondari Ngongongare iliyopo Wilayani Arumeru .


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36DT3f7
via

Post a Comment

0 Comments