OFISA JESHI LA POLISI ,WAFANYABIASHARA WATATU KORTINI WAKIKABILIWA NA MASHTAKA MATATU LIKIWEMO LA KULISABISHIA JESHI LA POLISI HASARA ZAIDI YASH. MILIONI 798.7

  Masama Blog      

Na Karama Kenyunko,Michuzo Blog.

OFISA wa Jeshi la Polisi, Emmanuel Mkilia (44) na wafanyabiashara watatu leo Januari 6,2020 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la  kulidanganya jeshi la polisi na kulisababishia hasara ya zaidi ya Sh M. 798.7.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni, Donald Mhaiki (39) mtaalamu wa masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na wafanyabiashara Abdi Ally (48) na Mohyadin Hussein (56) ambao wote kwa pamoja wamesomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salum Ally.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa na wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon akisaidiana na Wakili wa Serikali, Janeth Magoho imedai 1s,llęc7az3,2 wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka matatu ambayo ni kulisababishia jeshi la Polisi hasara, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha.

Katika shtaka la kwanza imedaiwa, kati ya Machi 19 na Oktoba 18,  2013 Jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao kwa pamoja walisababishia mamlaka (Jeshi la Polisi) hasara ya Sh 798,789,272.

Imeendelea kudaiwa kuwa, katika tarehe hizo na maeneo hayo ya jiji la Dar es Salaam, washitakiwa walijipatia toka jeshi la Polisi Sh 798,789,272 kwa kujifanya wameweka mfumo wa taarifa za watuhumiwa waliokamatwa na ambao wanashikiliwa (Arrest and Detention System) kwenye vituo nane na kutoa hati mbili zilizoonesha kwamba mfumo huo umewekwa kwenye vituo vinne huku wakijua kuwa sio kweli.

Katika shtaka la utakatishaji imedaiwa washitakiwa hao walijipatia fedha hizo wakati wakijua kuwa zimetokana na kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Hata hivyo, washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza wala kutoa dhamana kwa kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida zinasikilizwa Mahakama Kuu.

Hata hivyo, Wakili Wankyo alidai upelelezi wa kesi hiyo upo katika hatua za mwisho kukamilika hivyo, aliomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Ally ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 20, mwaka huu na washitakiwa walirudishwa rumande kwa sababu mashitaka hayo hayana dhamana kisheria.

Ofisa wa jeshi la polisi Emmanuel Mkilia aliyeko mbele na wenzake wakirudishwa mahabusu baada ya kesi yao ya kutakatisha fedha na kulidanganya jeshi la polisi ilipomalizika kusomwa. Watuhumiwa hao wamerudishwa rumande kwa kuwa mashtaka yao hayana dhamana


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2N0GtPe
via
logoblog

Thanks for reading OFISA JESHI LA POLISI ,WAFANYABIASHARA WATATU KORTINI WAKIKABILIWA NA MASHTAKA MATATU LIKIWEMO LA KULISABISHIA JESHI LA POLISI HASARA ZAIDI YASH. MILIONI 798.7

Previous
« Prev Post