Naibu Waziri Ulega atatua changamoto za wafanyabiashara Mnada wa Kimataifa wa Mifugo Pugu

  Masama Blog      

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akipewa maelezo ya mtambo uliokuwa ukitumika kwa kwa ajili ya kuteketeza mifugo iliyokufa katika Mnada wa Pugu wakati alipofanya ziara katika mnada huo na kuahidi kufanyia kazi katika ununuzi wa mtambo wa kuteketeza mifugo iliyokufa au mizoga.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akipewa maelezo na Meneja wa Mnada wa Mifugo Pugu Kerambo Samwel kuhusiana na mipaka ya Mnada wa Pugu wakati alipofanya ziara katika mnada huo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akipiga simu baada ya kukuta tatizo la maji katika mnada wa Pugu kwa Meneja wa Dawasa Kanda ya Ukonga.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akiangalia sehemu ya mradi wa maji ambao hauna maji wakati alipofanya ziara katika Mnada wa Pugu.
Maji ya Bwawa la Msimu linalotumika kunyweshea maji ambayo safi na salama.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akiangalia namna mbuzi wanavyohifadhiwa katika Mnada wa Pugu wakati alipofanya ziara kuangalia miundombinu katika mnada huo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akiwa katika Mzani kupimia mifugo ambao haufanyi kazi na kuahidi kuweka mzani mwingine katika kulinda maslahi ya mfugaji.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akimwagalia Ng’ombe wakati alipofanya ziara katika Mnada wa Mifugo Pugu jijini Dar es Salaam.
 

*Apiga simu kila mamlaka kutatua changamoto za utendaji katika Mnada wa Mifugo Pugu

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

WAFANYABIASHARA wa Mnada wa Kimataifa wa Mifugo Pugu jijini Dar es Salaam wamesema kuwa wamekuwa na changamoto katika soko hilo zinazojirudia kwa viongozi wanaofika hapo lakini hatua zimekuwa hazichukuliwi licha ya kuingiza mapato katika serikali.

Hatua hiyo imekuja mara baada Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega kutembelea miumdombinu ya Mnada huo ikiwa ni kuzungumza na wafanyabiashara hao katika kwenda na utatuzi wa kupiga simu kwa mamlaka zinazohusiana changamoto katika Mnada huo.

Kero zilizotolewa na wafanyabiashara hao kwa Naibu Waziri Ulega alizibeba na kutolea maamuzi hapohapo katika mamlaka kuanza kutekeleza ili wafanyabiasha wafanye kazi katika mazingira bora.

Naibu Waziri Ulega katika kero ya maji aliimaliza kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Dar es Salaam (Dawasa) kwenda kesho katika kuangalia miundombinu ya maji katika mnada huo.

Akizungumza katika Mnada huo amesema kuwa hawewezi kumuangusha Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kero ambazo anauwezo wa kutatua na kuahidi mambo yote yatafanyika na baada ya Bunge la Februari atafika kuangalia hali ya utekelezaji.

Ulega amesema kuwa ni marufuku kwa wafanyabiashara wan je nchi kununua mifugo katika minada midogo na kuwataka wakurugenzi wa nchi nzima kusimamia hilo ikiwa ni kulinda ajira za watu ndani katika biashara ya mifugo mbalimbali.

Aidha amesema kuwa miundombinu ya barabara itashughulikiwa na Tarura kutokana na mawasiliano alioyafanya na Mkurugenzi Mkuu wa Tarura kuhusiana na ujenzi wa barabara kutoka Gongolamboto hadi Pugu Mnadani.

Ulega amesema kuwa Manispaa ya Ilala ihakikishe inaboresha huduma katika Mnada huo kutokana na mapato wanayoyapata katika Mnada huo pamoja na kuahidi kufatilia utitiri wa leseni.

Meneja wa Mnada wa Mifugo Pugu Kerambo Samwel amesema kuwa mapato waliokusanya kuanzia Julai hadi Januari Mosi ni zaidi ya sh.bilioni 1.9 na mwaka 218/2019 walikusanya zaidi ya sh.bilioni Tatu.

Meneja huyo amesema kuwa wanakwenda kwa kasi katika mipango ya serikali ya kufikia lengo la ukusanyaji wa mapato au kuvuka malengo hayo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36kE8Xb
via
logoblog

Thanks for reading Naibu Waziri Ulega atatua changamoto za wafanyabiashara Mnada wa Kimataifa wa Mifugo Pugu

Previous
« Prev Post