MPANGO KABAMBE WA MATUMIZI BORA YA ARDHI YA KILIMO WAANDALIWA.

  Masama Blog      
Kikao kazi cha Kupitia ,Kuboresha na Kuhuisha Rasimu ya Mpango Kabambe wa Matumizi ya Ardhi ya Kilimo wa mwaka 2020 kimefanyika mjini Morogoro leo kwa lengo la wajumbe kutoa maoni yao ya kuuboresha .

Akizungumza wakati wa kikao kazi hicho Mkurugenzi Msaidizi Usimamizi wa Ardhi ya Kilimo Sospeter Mtemi amesema lengo la wizara ni kupata maoni ya wadau ili kuwa na mpango kabambe wa kuhakikisha ardhi ya kilimo inalindwa na kutumika kwa mujibu wa sheria kukuza sekta ya kilimo.

" Kukamilika kwa kazi hii  kutaifanya serikali kuwa na mpango kabambe wa kwanza nchini wa matumizi bora ya ardhi utakaotumika na taasisi zote za umma na binafsi kusimamia shughuli za kilimo" alisema Mtemi

Msisitizo unawekwa kwenye kukifanya kilimo kuchangia upatikanaji wa uhakika wa chakula ,biashara na kukuza ajira kwa watanzania kupitia mpango kabambe unaoandaliwa.

Kikao kazi kimeazimia kuwa rasimu ya mpango kabambe iwasilishwe kwa wadau wengi zaidi ili watoe maoni yao kabla ya kikao kingine kuitishwa.

Mchakato huu ulianza mwaka 2009 lakini ukasitishwa kutokana na ukosefu wa rasilimali fedha kuukamuilisha.

Kikao kazi hiki kiliandaliwa na wizara ya Kilimo na kushirikisha wizara zote za kisekta ikiwemo ,Mifugo na Uvuvi,Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira,Ofisi ya Rais Tamisemi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Wizara ya Ardhi,Wizara ya Maliasili na utalii na sekta binafsi wakiwemo MVIWATA.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/370sXmD
via
logoblog

Thanks for reading MPANGO KABAMBE WA MATUMIZI BORA YA ARDHI YA KILIMO WAANDALIWA.

Previous
« Prev Post