MOTO ULIOKUWA UNAWAKA ENEO LA KUHIFADHI MAFUTA KIGAMBONI WADHIBITIWA...DC AELEZEA HATUA KWA HATUA

  Masama Blog      
Na Said Mwishehe,Michuzi Globu

MKUU wa Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam Sarah Msafiri kuwa moto ambao ulikuwa unawaka katika Kampuni ya Lake Oil na kusababisha taharuki kubwa kwa wananchi tumefanikiwa kudhibitiwa na hakuna watu waliopoteza maisha.

Moto huo ulioanza kuweka jana usiku na kusababisha eneo la kuhifadhia mafuta la kampuni hiyo lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam ulisababisha hofu kwa wananchi na kuzua taharuki kubwa huku baadhi ya watu wakiamini moto huo utakuwa umeleta maafa yakiwemo ya watu kupotea maisha.

Akizungumzia moto huo ,Mkuu wa Wilaya hiyo ya Kigamboni Sarah Msafiri amesema anashukuru vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Lake Oil kwa kufanikisha kuudhibiti moto huo ambapo amesema baada ya moto huo kuanza kuwaka ilibainika kuna Valvo ya mafuta ambayo iko chini na inatakiwa kufungwa,hivyo vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na wafanyakazi waliofanikiwa kuifunga valvo hiyo .

"Kuna valvo ya mafuta ilikuwa inavuja kule chini na hivyo askari wetu walijitolea licha ya kuwapo na moto mkubwa na moshi kwenda kuifunga.Kuna askari mmoja aliamua kujitoa maisha yake kwa kwenda ilikokuwa ile valvo na akafanikiwa kuifunga na mafuta kuacha kuendelea kutoka.Anastahili pongezi kubwa kwa kujitoa kwake, moto umedhibitiwa na hakuna madhara yoyote kwa binadamu,amesema Msafiri.

Amesisitiza kwamba askari huyo mzalendo sio tu wamefanikiwa kuifunga valvo iliyokuwa inavujisha mafuta ,bali ujasiri wake umenisaidia kuokoa maisha ya maelfu ya Watanzania wakiwemo wanaishi Kigamboni pamoja kuokoa uchumi wa nchi sita ambazo itategemea mafuta yake kutoka eneo hilo.

Ametoa hofu wananchi kuwa hali kwa sasa ni shwari na hakuna moto tena katika eneo hilo tangu uliposhibitiwa huku akitumie nafasi hiyo kueleza wazi Kikosi cha Zima Moto nacho kimefanya kazi kubwa sana  kwa kushirikiana na vikosi vingine vya ulinzi na usalama.

Hata hivyo amesema baada ya moto huo kudhibitiwa watafuatilia kitaalam kujua chanzo cha moto kilikuwa nini licha ya kwamba kulikuwa na hiyo valvo iliyokuwa inavujisha mafuta ambayo imebainika awali.
 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2FyGmGC
via
logoblog

Thanks for reading MOTO ULIOKUWA UNAWAKA ENEO LA KUHIFADHI MAFUTA KIGAMBONI WADHIBITIWA...DC AELEZEA HATUA KWA HATUA

Previous
« Prev Post