Ticker

10/recent/ticker-posts

MNEC MWAKITINYA AONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA OFISI YA CCM, MILIONI 2.5 ZAPATIKANA


Charles James, Michuzi TV

VYAMA vya upinzani nchini vimetakiwa kufanyia marekebisho mfumo wao wa uongozi kabla ya kuomba ridhaa mbele ya watanzania ya kuongoza Nchi.

Kauli hiyo imetolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mwakitinya wakati alipokua akizungumza na wanachama na wafuasi wa chama hicho katika mkutano mkuu wa Matawi uliofanyika kata ya Ntyuka jijini Dodoma.Mwakitinya pia ameongoza harambee ya ujenzi wa ofisi ya tawi ya jumuiya ya wanaccm katika eneo walilopewa na viongozi wa kata ya Ntyuka .

Harambee hiyo ilifanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi Milioni 2.5 ambapo kiasi cha Sh Laki Sita kilipatikana hapo hapo huku pia vifaa kama Kompyuta, Milango, Misumari vikiwa kama ahadi.

MNEC Mwakitinya amewakumbusha wanachama na wanafunzi ambao ni wanachama wa CCM umuhimu wa kujenga chama chao na kukitumikia pamoja na kudumisha umoja na mshikamano kuelekea uchaguzi mkuu.

" Tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu niwaombe wanachama wenzangu wa CCM kuhakikisha tunamchagulia viongozi wenye weledi ambao watamsaidia kazi Mhe Rais Magufuli, tusichague bora viongozi bali viongozi bora.

Mhe Dk Magufuli amefanya kazi ya kutukuka ndani ya awamu yake hii ya kwanza, ni jukumu letu sisi vijana na wanachama wa CCM kwenda hadharani na kueneza makubwa yote yaliyofanywa na serikali yetu ya Hapa Kazi tu, tusimuache Rais aseme peke yake twendeni tukamsemee sisi," Amesema Mwakitinya.

Aidha amevitaka vyama vya siasa kuacha kulalamika kuhusu tume huru ya uchaguzi kwani tume iliyopo ndiyo ambayo imewapa wabunge wengi bungeni na madiwani hivyo wanapaswa kuiheshimu.

" Nawashangaa sana wapinzania wanalalamika wanatak Tume huru ya uchaguzi kana kwamba hakuna tume, maana kungekua hakuna tume huru kule bungeni kusingekua na wawakilishi wao au kwenye madiwani. Wao Tume inakua nzuri wakishinda, wakishindwa inakua mbaya," Amesema Mwakitinya.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mwakitinya akizungumza na wanachama na wanafunzi wanachama wa CCM katika mkutano wa kuendesha harambee ya Ofisi ya CCM Kata ya Ntyuka Wilaya ya Dodoma.
 Wanafunzi wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya CCM, Mussa Mwakitinya alipokua akizungumza nao kwenye harambee ya kuchagua ujenzi wa ofisi ya kata ya Ntyuka Wilaya ya Dodoma.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/35Q9d3M
via

Post a Comment

0 Comments