Ticker

10/recent/ticker-posts

MIKAKATI KABAMBE YAANDALIWA KUHAKIKISHA MAPATO YANAPATIKANA SOKO JIPYA LA MACHINJIO YA KUKU

MKURUGENZI wa Baraza la Manispaa ya Mjini Said Juma Ahmada, amesema tayari wameandaa mikakati kabambe ya kuhakikisha mapato yanapatikana katika soko jipya la machinjio ya kuku lilopo darajani mjini Unguja.

Hatua hiyo imetokana na agizo la Waziri wa Kazi,Uwezeshaji Wanawake na Watoto, Maudline Cyrus Castico  baada ya kuliagiza Baraza la manispaa Mjini Zanzibar kuhakikisha kuwa mapato yote yatayo kusanywa katika soko hilo yalipiwe kupitia njia ya benki ili kuepuka uvujaji wa mapato ya soko hilo.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa Soko jipya la kisasa la kuku ikiwa ni shamra shamara za sherehe za  kutimiza miaka 56 ya mapinduzi ya Zanzibar ambapo alisema baraza hilo pia lina mikakati ya kuhakikisha eneo lote la mjini linakuwa safi muda wote.

Alisema mikakati mingine ni kuwa Baraza la Manispaa limejipanga kufanya kazi ipasavyo kwani juhudi zao zinatambuliwa na kuthaminiwa na wananchi.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa Baraza hilo halitarudi nyuma na kwamba itahakikisha masoko yote yatatengenezwa katika mifumo ya kisasa i  inayo kubalika duniani bila yakuangalia maeneo au pahala lilipo.

Alisema uzinduliwaji wa baraza hilo ni kutimiza ilani ya CCM ya mwaka 2015 hadi 2020 ikiwa ni kuona Manispaa ni sehemu ya ugatuzi wa madaraka mikoani.

"tayari tumeshajipanga kujenga majengo mapya na ya kisasa na masuala mengine ya nayo fanana na hayo hivyo utunzaji wa pesa utazingatiwa kuepuka uvujaji wa mapato hayo ili malengo ya manispaa yafikiwe kwa urahisi,"alisema

Akitoa agizo hilo baada ya uzinduzi wa soko hilo Waziri wa Kazi,Uwezeshaji Wanawake na Watoto, Moudline Scyras Castico aliwataja Baraza hilo wapunguze kutegemea Hazina na kwamba wajenge utamaduni wa malipo ya pesa za soko la kuku kulipia njia za benki.

Waziri huyo alisisitiza kuwa malengo yao yatatimia iwapo pale malipo ya kodi na makusanyo mengine yatalipiwa moja kwa moja benki kwani ndiko kwenyedhamana ya utunzaji wa fedha za Serikali na mashirika.

Alisema baraza hilo lina kazi nyengine za Manispaa ya kuingia mfumo wa ubia na watu binafsi kwa masuala yanayo wezekana kwani kufanya hivyo ni kutoa fursa ambazo hitajika na kulifanikisha baraza linajiendesha wenyewe.

Hata hivyo alisema kuwa katika pesa hizo wanapaswa kupanga bajeti za kulifanyia marekebisho soko kila pale itapo hitajika na wasisubiri soko hilo kuharibika na kurudisha hadhi ya zamani.

Naye Naibu Katibu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Tawala za Mikoa Idara Maalum za SMZ Khalid Abdalla Omar alisema kuwa ujenzi wa mradi wa soko hilo ulianza katika kipindi cha mosi Septemba mwaka 2018 na hatimaye umemalizika 25 Januari mwaka 2019 ambapo zaidi milioni 200 zilitumika hadi kumaliza kwake.

Alisema kuwa soko litawahudumia Wafanya Biashara 120 hali ambayo ni dhahiri itaongeza mapato.


WAZIRI wa Kazi,Uwezeshaji Wanawake na Watoto, Mhe.Maudline Cyrus Castico akikata utepe katika uzinduzi wa soko la kisasa la kuku katika eneo la darajani Unguja.

MKURUGENZI wa Baraza la Manispaa ya Mjini Said Juma Ahmada, akizungumzia mikakati ya manispaa ya mjini katika kuimarisha majukumu yake kwa wananchi mara baada ya kuzinduliwa soko hilo.
BAADHI ya Wananchi na Viongozi mbali mbali wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa soko la kisasa la kuku lililopo darajani Unguja.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36CVizq
via

Post a Comment

0 Comments