MGANGA WA KIENYEJI ATUHUMIWA KUMBAKA MGONJWA WAKE

  Masama Blog      
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limemkamata na linaendelea kumshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Hemed Jumanne (40) mkazi wa Sengerema,anayedaiwa kuwa Mganga wa Kienyeji,kwa tuhuma za kumbaka Mwanamke mmoja (jina kapuni) (32) mkazi wa Butimba

Tukio hilo limetokea Januari 4,2020 katika mtaa wa Jiwe,Kata ya Igogo Wilaya ya Nyamagana,hii ni baada ya Muathirika wa tukio hilo kufika kwa Mganga Tajawa hapo juu kwa lengo la kupata tiba ya maradhi yanayomsumbua,ndipo Mganga huyo aliingiwa na tamaa ya Kimapendi na baadae alimpa dawa za kumpumbaza kisha kumbaka kwa  kuweka baadhi ya dawa za Kienyeji  sehemu za siri za Mwanaume (Mganga) na baadae kuingiza sehemu za siri za Mwanamke kama sehemu ya matibabu.

Kitendo hiki cha kikatili cha kubaka hakivumiliki,ni cha Kinyama na ni kosa la Jinai.

Mtuhumiwa huyo atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo,na Muathiriwa tukio hilo ametibiwa hospitali na hali yake inaendelea vizuri,kwani ameruhusiwa kutoka.Jeshi la Polisi linatoa wito kwa Wananchi kujiepusha na Makundi ya Wahalifu  wanaotumia Mwamvuli wa Uganga wa Jadi kutapeli Watu na kufanya vitendo vingine vya kijinai  from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36AC0KY
via
logoblog

Thanks for reading MGANGA WA KIENYEJI ATUHUMIWA KUMBAKA MGONJWA WAKE

Previous
« Prev Post