MBUNGE PROFESA MUHONGO AKABIDHI ZAWADI ZA VIKOMBE, FEDHA KWA WASHINDI WA KUPIGA KASIA MUSOMA VIJIJINI Inbox x

  Masama Blog      

Mbunge wa Jimbo la la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo akimkabidhi zawadi ya Kombe la ushindi katika mashindano ya kupiga kasia yaliyofanyika katika Ziwa Victoria Kijiji cha Bukima,Musoma Vjijini mwishoni mwa mwaka 2019.
Mmoja wa washindi wa mashindano hayo (kulia), akipongezwa kabla ya kukabidhiwa kombe la ushindi wa mashindano ya hayo ya kupiga kasia.
Mmoja wa washindi akikabidhiwa zawadi ya Kombe huku akiashangiliwa na wenzake.
Baadhi ya washiriki wa mashindano hayo

Wananchi wakishuhudia mashindano hayo.Na Mwandishi Maalumu

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo amekabidhi zawadi za vikombe na fedha taslimu kwa washindi wa mashindano ya Kupiga Kasia (The Annual Boat Race) yaliyofanyika mwishoni mwaka jana katika Kijiji cha Butima, Ziwa Victoria jimboni humo.

Mbunge wa Jimbo la la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ameamua kwa vitendo kufufua Utamaduni na Michezo jimboni mwao iliyokuwa inafifia na kuanza kutoweka., ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020, jimboni humo.

Kila Mwaka, Mbunge huyo anatayarisha na kufadhili MASHINDANO ya KWAYA (nyimbo) na NGOMA ZA ASILI.

Vilevile, Mbunge huyo ni mmoja wa WAFADHILI wa Timu ya Mpira ya Mkoa wa Mara, BIASHARA UNITED inayoshiriki Ligi Kuu ya Taifa. Ameombwa na kukubali kuna mmoja wa Wafadhili wa WASAGA FC ya Kata ya Nyamrandirira itakayoshiriki Ligi ya Daraja III. Mbunge huyo alishagawa Vifaa vya Michezo Vijijini na Mashuleni.

MASHINDANO YA KUPIGA KASIA 2019 (The Annual Boat Race) - Washindi na Zawadi


Mbunge wa Jimbo ametoa ZAWADI hizi:


MSHINDI 1


Kata ya Murangi


Tsh Milioni 1 & Kikombe


MSHINDI 2

Kata ya Musanja

Tsh 700,000 & Kikombe


MSHINDI 3

Kata ya Suguti

Tsh 400,000 & Kikombe


Mshindi wa Nne

Kata ya Bukima


Mshindi wa Tano

Kata ya Rusoli

ZAWADI ndogo ndogo nazo zilitolewa.

Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wameomba Mbunge wa Jimbo lao AENDELEE kutayarisha MASHINDANO ya kupiga KASIA na ikiwezekana yafanyike mara pili kwa Mwaka.

Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha MATUKIO mbalimbali ya Mashindano ya kupiga Kasia yaliyofanyika Kijijini Bukima, jana, tarehe 30.12.2019.

SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MBUNGE WA JIMBO

"MWAKA MPYA (2020) uwe ni Mwaka wa Maarifa mapya, Ubunifu mkubwa, Ushirikiano mkubwa, na Utekelezaji wenye umakini na ufanisi mkubwa.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/35krsOR
via
logoblog

Thanks for reading MBUNGE PROFESA MUHONGO AKABIDHI ZAWADI ZA VIKOMBE, FEDHA KWA WASHINDI WA KUPIGA KASIA MUSOMA VIJIJINI Inbox x

Previous
« Prev Post