MAVUNDE AFANYA MKUTANO WA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI JIMBONI MWAKE

  Masama Blog      
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amefanya mkutano wa kusikiliza kero za wananchi wa kata ya Ntyuka ambapo ameeleza mikakati na mipango iliyopo kwenye utatuzi wa kero za msingi katika Kata hiyo;

1.BARABARA YA NTYUKA-MVUMI-CHOLOLO

Barabara hii itajengwa kwa kiwango cha lami na kwa mwaka 2019/2020 imeshatengewa fedha kwa ajili usanifu wa kina na upembuzi yakinifu.

Mh Rais Dr John Pombe Magufuli ameshatoa maagizo kwa TANROAD kuanza kujenga kwa kiwango cha Lami kipande cha kuanzia Chamwino Ikulu mpaka makao makuu ya Jeshi eneo plna Chololo-Kikombo.

Hivyo kwa mwaka huu 2020/2021 tunapeleka maombi ya fedha za kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

2.BARABARA ZA NDANI ZA NTYUKA

Nimempa maelekezo Meneja wa TARURA Dodoma Eng.Mkinga tuongozane pamoja kuzitembelea barabara hizo na kuzipatia ufumbuzi kero hizo za barabara hasa za maeneo ya Bwawani na Makaburini.

Kazi hii inafanyika ndani ya siku chache kuanzia tarehe 01.01.2020.

3.MAJI
Maeneo ya katikati ya Ntyuka na pembezoni yanakabiliwa na ukosefu wa maji na maeneo mengine msukumo wa maji ni mdogo hivyo kushindwa kuwafikia wananchi wote kwa wakati.

DUWASA wamemaliza kufanya mazungumzo na UDOM ili pia kutumia mfumo wa maji uliopo hapo chuoni kusaidia msukumo wa maji mkubwa utakaoenda sambamba na uwekaji wa miundombinu ya usambazaji wa Maji katika eneo lote la Ntyuka.

5.UMEME
Kata ya Ntyuka itanufaika na mpango wa usambazi wa nishati ya umeme katika maeneo 34 ya Jiji ambayo yamesalia kuungwa na Nishati ya umeme.

Kiasi cha Tsh 50bn kimetengwa na TANESCO kukamilisha maeneo yaliyobaki ikiwemo Ntyuka.

6.UPIMAJI MAENEO

Zoezi la Upimaji katika kata ya Ntyuka ilikuwa ni kero kubwa,Kampuni ya Upimaji imepatikana chini ya usimamizi wa Jiji ambapo sasa zoezi la utambuzi wa wananchi na maeneo yao limekamilika kwa awamu ya kwanza.Muda sio mrefu wananchi watamilikishwa maeneo yao kwa mujibu wa sheria.

7.MGOGORO WA ARDHI YA YALIYOKUWA MASHAMBA YA WANANCHI UDOM

Mgogoro huu upo katika ngazi ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya utatuzi wake hivyo tunasubiri maelekezo ya Serikali katika eneo hili.


 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36rq8Lh
via
logoblog

Thanks for reading MAVUNDE AFANYA MKUTANO WA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI JIMBONI MWAKE

Previous
« Prev Post