Matumla ampigisha tizi Mtango kwa saa 6 Dar

  Masama Blog      
Na Ripota wetu,Michuzi Blog

Katika kuonyesha amedhamiria kubakisha ubingwa wa dunia wa UBO nyumbani, Rashid Matumla ambaye ni kocha wa bondia Salim Mtango amemtengeneza programu kali kali bondia huyo ikiwamo kufanya mazoezi kwa saa 6 kila siku kwenye kambi yake ya Dar es Salaam.

Mtango atamkabiri Suriya Tatakhun wa Thailand Januari 31 kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Mtanzania huyo ameanza kambi jijini Dar es Salaam ambako kwa mujibu wa ratiba yake anajifua kwa saa 6 kila siku.

"Nafanya hivi ili kujiweka fiti nafanya mazoezi tofauti tofauti ikiwamo ya mbinu, ufundi na sparing, natambua ugumu wa pambano langu, ubora wa mpinzani wangu na ndoto zangu ni kubakisha ubingwa nyumbani.

Kocha Rashid Matumla ambaye pia ni bingwa wa zamani wa dunia wa WBU alisema hana shaka na maandalizi ya Mtango, kwani amemuandalia mbinu za mauaji.

"Nahitaji awe bingwa wa dunia na kufuata nyayo zangu, bahati nzuri si mvivu wa mazoezi, amekuwa akifanya kile anachoelekezwa," alisema.

Promota wa pambano hilo, Ally Mwanzoa alisema maandalizi yanakwenda vizuri ikiwamo mpinzani wa Mtango kuwasili nchini wiki hii akitokea Thailand.

"Atakapowasili bondia huyo atafanya mazoezi ya wazi kabla ya kukutanishwa na Mtango kwa mara ya kwanza, zoezi litakalofanyika siku chache kabla hawajapima uzito," alisema Mwanzoa.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2v6ayqN
via
logoblog

Thanks for reading Matumla ampigisha tizi Mtango kwa saa 6 Dar

Previous
« Prev Post