MAJAMBAZI WATANO WAUWAWA WAKATI WAKIRUSHIANA RISASI NA POLISI JIJINI ARUSHA

  Masama Blog      
.Kamanda wa Polisi mkoani hapa Jonathan Shana akiongea na vyombo vya habari mkoani hapa kuelezea tukio la kuuwawa kwa majambazi wa Tano wakiwa njiani kuelekea kwenye tukio la uporaji wilayani Simanjiro na kuanza kushambuliana na Polisi eneo la Mateves kata ya Olmot wilayani Arumeru picha na Ahmed Mahmoud Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiongea na waandishi wa habari kulipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri wanaoifanya kwa kipindi cha mwaka mzima nakuufanya mkoa kuwa shwari kwenye makao makuu ya Jeshi hilo mkoani hapa picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.
Sehemu ya bunduki aina ya shotgan na bastola zikiwemo na risasi 8 na magazine mbili za bastola zenye risasi 7 na 1 zilizokutwa kwenye tukio ikiwemo na simu mbili ambazo walipora kabla ya kwenda kwenye tukio wilayani simanjiro picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana akiangalia Pikipiki ambazo walikuwa wakisafiria majambazi hao waliouwawa na jeshi hilo baada ya majibizano ya risasi kwenye eneo la mateves kata ya Olmot jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha
Mmoja ya wananchi ambaye aliporwa simu yake akiwa nyumbani kwake pamoja na bunduki aina ya shotgun ya mumewe wakiongea na kulisifu jeshi hilo kwa kupatikana kwa simu yake ndani ya muda mfupi mbele ya waandishi wa habari kutoka vyomboi mbalimbili mkoani hapa picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
 
 
N Woinde Shizza,Arusha


Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Jonathan Shanna amesema kikosi cha jeshi la polisi Mkoani humo kimewaua majambazi sugu watano wakati wakijibizana risasi na polisi na kuwakuta na silaha aina ya Shotgun Pump Action 32265,Chinese Pistol,Bastola 1 bandia,risasi 11 pamoja na simu 2 & pikipiki 3.

Kamanda Shanna amesema msako unaoendeshwa na Jeshi la Polisi hautaishia hapo, na watahakikisha kuwa tabia za kuvuna pasipo kupanda zinazofanywa na vikundi vya watu wachache ndani ya mkoa huo zinadhibitiwa.

Amesisitiza kuwa jiji la Arusha litakuwa shwari, na akionya kuwa wale wote wanaofanya vitendo vya uhalifu wataangukia mikononi mwa Polisi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuzidi kuimarisha ulinzi na usalama katika jiji hilo. Pia amechukua nafasi hiyo kutuma salamu na kumpongeza Waziri mpya wa Mambo ya ndani Mhe. George Simbachawene kwa kuanza kazi vizuri.

"Sisi kama mkoa tutashirikiana na Wizara yake ya Mambo ya Ndani kuona namna ya kuwapa zawadi Askari hawa waliyofanikisha jambo hili (la kuwaua majambazi sugu 5) maana wamenifanya niwe na furaha sana". Amesema RC Gambo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2UcUjT2
via
logoblog

Thanks for reading MAJAMBAZI WATANO WAUWAWA WAKATI WAKIRUSHIANA RISASI NA POLISI JIJINI ARUSHA

Previous
« Prev Post