Madiwani Tandahimba wapitisha bajeti ya Bilioni 28.7

  Masama Blog      
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Tandahimba wamepitisha bajeti ya zaidi ya Bilioni 28.7 kwa mwaka 2020/2021

Fedha hizo zimetokana na  vyanzo  vyake vya ndani ,ruzuku kutoka Serikali kuu,Wahisani pamoja na michango ya jamii

Akisoma bajeti hiyo Mweka Hazina wa Halmashauri ya Tandahimba Ally Machela alieleza Halmashauri  imejiwekea lengo la kukusanya zaidi ya shilingi Bil 5  Sawa na ongezeko la asilimia 23

"Ukilinganisha  na makisio ya mwaka 2019/2020  na mwaka wa fedha 2020/2021 ni ongezeko la asilimia 23,"alisema Machela.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Namkulya  Namkulya aliipongeza bajeti hiyo kwa kuweza kufikia vijiji  kwa kiwango kikubwa tofauti na miaka ya nyuma

"Naipongeza bajeti ya mwaka 2020/2021 imefikia vijiji kwa asilimia 85 haya ni mafanikio makubwa kwa Wilaya yetu,"alisema Namkulya
 Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Namkulya Namkulya akielezea jambo
 Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba aliwapongeza madiwani kwa kupitisha bajeti ya shilingi Bil 28.7 kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Tandahimba

 Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Tandahimba wakisikiliza Bajeti
Wakuu wa Idara wakisikiliza  maoni ya madiwani kabla ya kuipitisha


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2GtELlR
via
logoblog

Thanks for reading Madiwani Tandahimba wapitisha bajeti ya Bilioni 28.7

Previous
« Prev Post