Madiwani mjini Njombe walilia mipango ya kutokomeza ziro kwenye elimu

  Masama Blog      

Abuu Mtamike wa kata ya Mjimwema akichangia hoja katika baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Njombe lilofanyika katika ukumbi mdogo wa halmashauri,alipopata nafasi ya kuchangia mara baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya kamati ya kamati ya afya uchumi na elimu


Baadhi ya madiwani na wataalamu wa halmashauri ya mji wa Njombe wakiwa makini wakati wa kusikiliza taarifa za kamati za madiwani wa halmashauri hiyo.Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akitoa salamu za serikali katika baraza la madiwani lililofanyika hii leo mjini Njombe.
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Iluminatha Mwenda akifafanua jambo wakati wa kikao cha baraza la madiwani.


Na Amiri kilagalila-Njombe

Jitihada za makusudi zimetakiwa kuchukuliwa ili kuondoa sifuri na daraja la nne kwenye mitihani ya kidato cha nne katika shule za halmashauri ya mji wa Njombe licha ya halmashauri hiyo kushika nafasi ya pili kwa ufaulu katika mkoa wa Njombe.

Katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya mji wa Njombe baadhi ya madiwani akiwemo Abuu Mtamike wa kata ya Mjimwema,Filoteus Mligo diwani wa kata ya Lugenge na Reginald Danda toka kata ya Iwungilo wamesema wao kama madiwani wamekuwa wakihamasisha jamii kutekeleza yale yanayowapasa katika kukuza elimu hatua ambayo inapaswa kuungwa mkono na serikali kwa kupeleka fedha za maendeleo na kununua madawati badala ya kusalia wakipongezana kwa kushika nafasi ya pili kimkoa.

“Leo madiwani tukiwauliza kuna pesa yoyote ambayo imetoka serikalini kusapoti shughuli za elimu,leo utakuta bado huko kwenye kata kuna maboma tu,halafu tunakuja kusifiana tuko juu,hatuko juu kwasababu ya sifa zaidi ya kupambana,kujifunza ni hatua sio kukurupuka lazima kiwe na mwanzo,kwa hiyo kama hatujajipanga kwenye shule za misingi basi atakayepata ziro ni yule atakayeenda kidato cha kwanza”alisema Filoteus Mligo

Awali akitoa salaam za serikali mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amesema halmashauri ya mji wa Njombe licha ya kufanya vizuri bado inapaswa kuongeza nguvu katika sekta ya elimu kwani bado kuna wanafunzi wanafeli mitihani yao.

“Elimu ni msingi wa maisha na katika mtazamo mkubwa wa taifa hili kwenda uchumi wa viwanda ni lazima tuhakikishe kwamba watoto wetu wanasoma,ninachoamini halmashauri ya mji wa Njombe mnaweza mkafanya vizuri zaidi ya hapa” alisema Ruth Msafiri

Mwenyekiti wa kamati ya afya uchumi na elimu katika halmashauri hiyo Yurick Msemwa ambaye ni diwani wa kata ya Luponde amesema ili kupandisha kiwango cha ufaulu zaidi,mshikamano wa pamoja unahitajika kwa kila mmoja ndani ya halmashauri hiyo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Iluminata Mwenda amesema wamelazimika kuanzisha kampeni ya kuondoa zero katika shule zote kwa kuboresha miundombinu ya elimu na mbinu za ufundishaji.

“Tumefanya tathmini ya kidato cha nne mimi na wataalamu wangu na wakuu wa shule katika shule zetu za sekondari zilizopo ili kuona ni jinsi gani tunaweza kupunguza division IV,sisi ziro na IV zinatukera sana ndio sababu tumeanzisha operation ondoa F”alisema Iluminata Mwenda

Katika matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2019 halmashauri ya mji wa Njombe imeshika nafasi ya pili kimkoa ikiongozwa na halmashauri ya mji wa makambako hatua ambayo imewafanya madiwani hao kuona ulazima wa kupambana ili kufuta zero na daraja la nne katika shule zote.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2GFVClC
via
logoblog

Thanks for reading Madiwani mjini Njombe walilia mipango ya kutokomeza ziro kwenye elimu

Previous
« Prev Post