Ticker

10/recent/ticker-posts

LEO NI KUMBUKUMBU YA KUZALIWA SHAABAN ROBERT, MWANDISHI NGULI WA FASIHI YA LUGHA YA KISWAHILI.

Tarehe kama ya Leo ya 1909, yaani 01-01-1909 katika kijiji cha Vibambani, kata ya Machui katika Jiji(kwa sasa) la Tanga alizaliwa Mshairi na Mtunzi Mashuhuri wa Riwaya za Kiswahili.

Ingawa hakuna vyanzo vya kutosha juu ya maisha ya Utotoni ya Shaaban Robert lakini masimulizi yanaeleza alianza kazi kama Karani kwenye Serikali ya Kikoloni mara baada ya kumaliza Darasa la 11. Ndani ya Serikali ya kikoloni alihudumu kama  Karani, Afisa forodha(Bandari za Pangani na Bagamoyo), Ofisa-Mbuga ya Wanyama, Ofisi ya Vipimo na Ramani na hatimaye Idara ya Mipango!

Kwa nyakati tofauti alioa, wake watatu. Na kujaaliwa watoto kadhaa.

Pengine Shaaban Robert ndio mtunzi mashuhuri zaidi wa kazi za Fasihi ya Lugha ya Kiswahili. Aliandika Miswaada mbalimbali ya Mashairi, Insha na Riwaya(Mpaka hivi karibu, barua na insha zake zinachapishwa). Anajulikana kama Shakespeare wa Fasihi ya Kiswahili.

Miaka 58 baada ya Kifo chake bado kazi zake zinaakisi maisha ya sasa. Jina lake limebaki kwenye miadhara ya lugha ya Kiswahili na Magazetini. 

Ingawa aliandika tangu miaka ya 1920 lakini kazi yake ya kwanza ilitoka katika gazeti "Mamboleo" mwaka 1932, ikiwa ni barua kwa Mhariri wa Gazeti hilo, kazi hii iliitwa "Hirizi ya shilingi Mia" katika Barua hii Shaaban Robert alikemea tabia za Ushirikina au Shirki

Shaabani Robert alifariki Dunia, tarehe 22-06-1962 kwa Ugonjwa wa Moyo na kupungukiwa Damu akiwa na Umri wa Miaka 53 tu. Alizikwa Kijijini kwao Vibambani, Tanga.

Baadhi ya kazi alizoziandika au kuzitunga na kuacha Miswaada ni.....

1.Almasi za Afrika ( 1971)

2.Koja la Lugha(1969)

3. Insha na Mashairi(1967)

4.Kielezo cha Fasihi(1962)

5. Pambo la Lugha(1968)

6.Ashiki Kitabu Hiki (1968)

7. Mashairi ya Shaaban Robert (1971)

8. Sanaa ya Ushairi(1972)

9. Mwafrika Aimba(1969)

10. Masomo yenye Adili (1959) 

11.Mapenzi bora(1969) 

12.Tenzi za Marudi Mema na Omar Khayyam (1973) 

13. Utenzi wa Vita vya Uhuru (1961) 

14. Almasi za Afrika na Tafsiri ya kiingereza (1960)

15. Maisha yangu na baada ya miaka hamsini(1949)

16. Adili na Nduguze(1977) 

17. Kusadikika (1951)

18. Kufikirika(1968)

19.Wasifu wa Siti Binti Saadan(1967), binafsi nakipenda sana hiki kitabu!

20. Utu Bora Mkulima (1968)

21. Siku ya Watenzi wote(1968)

22. Barua za Shaaban Robert (1931-1958(2002)

23. Kielezo cha Insha(1954)

24. Methali na mifano ya kiswahili (2007)

Baada ya Kifo chake, Rais wa Tanganyika (wakati huo) aliutangaza mtaa wa Burton Street kuitwa Mtaa wa Shaaban Robert mwaka 1963.

Shaaban Robert ametunukiwa Tuzo na Vyeti mbalimbali kutokana na mchango wake kukuza fasihi na lugha ya Kiswahili.

Pamoja na Uwezo wake wa kuchagua maneno na msamiati bora wa Kiswahili lakini pia Shaaban Robert alikuwa na ujuzi mkubwa katika kuandika Lugha ya Kiingereza. Ushaidi wa Barua alizoandikia rafiki zake unadhihirisha hili.

Hivyo basi, tunaposisitiza Matumizi ya Kiswahili tusisahau Kiingereza kwani Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere  alipata kusema "Kiingereza ndio Kiswahili cha Ulimwengu"

Kheri ya Mwaka Mpya!

Francis Daudi 
0768035253



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2FdTEZ4
via

Post a Comment

0 Comments