KITABU CHA VISION NEVER DIE CHAZINDULIWA JIJINI DAR, MAUZO KUNUNUA KIWANJA CHA KUJENGA KANISA

  Masama Blog      
ASKOFU Stella Matte azindua kitabu ambacho kitawafungua watu kufikia malengo ya maono yao. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam Askofu Stella amesema kuwa kitabu hicho kinachoitwa VISION NEVER DIE kitawaongoza watu katika kufikia malengo ya maono yao wa kikisomwa mwanzo hadi mwisho kama mwongozo wa kufikia kile Mungu ameweka moyoni mwa kila asomae kitabu hicho.

Amesema kuwa maono ambayo hutambuliwa na Mungu hapa dunini hayafi hivi hivi mpaka yatimizwe.

Akizungumza wakati wa kuzindua kitabu hicho amesem vitabu vitauzwa na mapato yatakayopatikana yatakuwa kwaajili ya kununua kiwanja cha kujenga kanisa kwaajili ya kuhudumia taifa la Mungu.

Askofu Stella Matte amesema ukiwa na maono lazima uwenna bidii katika kufikia mafanikio ya maono yako, maono lazima yalindwe pamoja na kuto kuwashirikisha wengine maono yako mpaka waone matunda ya maono hayo amayo Mungu ameweka ndani yako.

Kitabu hicho kitauzwa kwa watu wa rika zote kwani kimefata miongozo ya uandikaji wa vitabu hapa nchini na kimetarajia kuelimisha watu katika kufikia malengo ya maono yao.

Hata hivyo Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, amesema kuwa katika biblia Mwenyezi Mungu alimshirikisha mtu mmoja katika maono hivyo maono wanayo wachache.

Kadogosa amesema maono kama Mungu amekushirikisha hayatakufa hivi hivi ni lazima yafanikishwe ili watu waweze kuona matokeo ya maono yako.

Amesema kuwa makusudi ya Mungu yanakamilika katika kumaliza au kukamilisha maono yaliyokusudiwa.

Hata hivyo amesema kuwa taifa lisipokuwa na maono haliwezi kufikia linakoenda ndio maana tunaona taifa letu linakoenda kwakuwa kunamtu ambaye amepewa maono na Mwenyezi Mungu.
Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, akifungua utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha Askofu Stella Matte, kitabu chenye jina la Vision Never Die ambacho kitalenga kukamilisha ndoto za watu waakao soma kitau hicho, Katikati ni Askofu, Stela Matte na Kushoto ni Dk. Asokile 
Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, akionesha kitau cha Askofu Stella Matte mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Katikati ni Askofu Stella Matte, ma kushoto ni Dk. Asokile.
Askofu, Stelle Matte, akimpa vitabu moja ya aliyenunua vitabu hivyo katika uzinduzi uliofanyika Mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Askofu Stella Matte, akizungumza kabla ya kuzinduz kitabu chake cha Vision Never Die. kitabu kilichozinduliwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, akizungumza wakati wa kuzindua kitabu chenye kukamilisha maono ya watu. Kitabu hicho kinachoitwa Vision never die ni kitabu ambacho kitaweza kusaidia watu wengi zaidi kujua maono yao na matokeo ya maono yao.
Mke wa Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa kulia, Martha Kadogosa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Vision Never Die kilichozinduliwa jijini Dar es Salaam wikiend hii. kushoto ni Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa.

Askofu, Stella Matte akikabidhi vitabu mara baada vya kuzinduliwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya waliohudhulia katika uzinduzi wa kitabu cha Vision Never Die jijini Dar es Salaam.

Salamu.
Dk. Asokile akizungumza na kufafanua kitau cha Askofu Asokile jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.from MICHUZI BLOG https://ift.tt/38hVh4e
via
logoblog

Thanks for reading KITABU CHA VISION NEVER DIE CHAZINDULIWA JIJINI DAR, MAUZO KUNUNUA KIWANJA CHA KUJENGA KANISA

Previous
« Prev Post