KIGWANGALLA, MKENDA SASA KAZI TU, WAKUTANA MWANZA

  Masama Blog      
 
Baada ya kumaliza tofauti zao ndani muda uliotolewa na Mhe. Rais, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla alikutana na  Prof. Adolf Mkenda, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo jijini Mwanza.

Viongozi hao wamekutana jana tarehe 08/01/2020 kwa ajili ya maandalizi kikao cha tatu cha maandalizi ya maonyesho ya Utalii kwa mikoa ya kanda ya Ziwa, Kigoma na Tabora pamoja na jukwaa la uwekezaji katika sekta ya utalii kwa Kanda Ziwa.

Pamoja na majadiliano ya maandalizi hayo, pia walipata fursa ya kupata kikombe cha Kahawa pamoja ambapo kwa sasa viongozi hao wamedhamilia kufanya kazi za kumsaidia Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2NbhRn3
via
logoblog

Thanks for reading KIGWANGALLA, MKENDA SASA KAZI TU, WAKUTANA MWANZA

Previous
« Prev Post