Ticker

10/recent/ticker-posts

KESI YA UHUJUMU UCHUMI NA UTAKATISHAJI FEDHA INAYOMKABILI ERICK KABENDERA YAENDELEA LEO,UAMUZI WA KUSHIRIKI MAZISHI YA MAMA YAKE AU LAH..KUJULIKANA BAADAE.

Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha inayomkabili Mwandishi wa Habari za uchunguzi Erick Kabendera umepinga mshtakiwa huyo kuruhusiwa kwenda kushiriki ibada ya mazishi ya mama yake mzazi, Verdiana Mujwahuzi aliyefariki hivi karibuni.

Hatua hiyo leo Januari 20,2020 wakati kesi hiyo ilipoitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa na wakili wa Kabendera, Gebra Kambole kuwasilisha maombi mahakamani hapo.

Mapema wakili Kambole ameiomba mahakama hiyo imruhusu Kabendera akashiriki Ibada ya Mazishi ya Mama yake mzazi katika Kanisa la Roman Katoliki lilipo Chang'ombe  leo mchana akidai kuwa suala la kushiriki sala ya mwisho ya msiba ni haki ya Binadamu, suala la faragha.

Amedai, kushindwa kuudhuria maziko ya Mama yake atakuwa ameadhibiwa adhabu kubwa tena kwa kuangalia uhusiano wa mshitakiwa na mama yake mzazi kwani alikuwa akimuuguza hivyo ni vizuri akatoa heshima ya mwisho

Wakili Jebra amedai kuwa ni muhimu kwa Kabendera kushiriki kwa sababu Mama mzazi ni mmoja, akifa anaagwa mara moja.

"Jamhuri haitaathirika kwa lolote kwa sababu mshitakiwa atakuwa chini ya ulinzi na ibada itakuwa mchana kanisani na Temeke sio mbali na gerezani, tunaomba akatoe heshima ya mwisho," ameomba.

Akijibu home hizo, wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amemueleza Hakimu Mkazi, Janeth Mtega anayesikiliza kesi hiyo kwamba Jamhuri inampa pole Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi.

"Hata sisi tuna masikitiko makubwa na tunampa pole nyingi Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi, lakini mahakama isifungwe mikono kwa maombi yaliyowasilishwa ya kutaka kushiriki msiba, akiongeza Kudai kuwa, maombi ya Kabendera kupitia mawakili wake yamewasilishwa wakati ambao si sahihi kwa sababu mahakama haina mamlaka na DPP hajaipa kibali ya kusikiliza kesi hiyo.

"Katika macho ya kisheria mahakama yako haina mamlaka, hata sisi tuna masikitiko makubwa lakini mahakama isifungwe mikono," amesema.

Kuhusu mwenendo wa kesi, upelelezi unaendelea na shauri limefika hatua nzuri baina ya mshtakiwa na  (DPP).

Kufuatia home hizo, Hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi saa 8:45 mchana huu kwa ajili ya kutoa uamuzi kama Kabendera ashiriki Ibada ya mazishi ya Mama yake mzazi ama lah.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/35iHjgL
via

Post a Comment

0 Comments