KESI YA KABENDERA YAAHIRISHWA HADI FEBRUARI 10

  Masama Blog      
 Na Karama Kenyunko globu ya jamii.


UPANDE wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili, mwandishi wa Habari za uchunguzi Erick Kabendera, umeieleza Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu kuwa, mchakato wa makubaliano kati ya Kabendera na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) bado unaendelea.

Wakili wa Serikali Gloria Mwenda amedai hayo leo Januari 27,2020 Mbele ya Hakimu Mkazi, Jenet Mtega wakati kesi hiyo ilipokuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Mwenda amedai upelelezi bado unaendelea na mchakato wa makubaliano kwa DPP pia unaendelea hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

 Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 10 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa Sh.Mil 173.

Inadaiwa kuwa katika kipindi hicho, Kabendera alijihusisha na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Inadaiwa kuwa katika kipindi hicho,bila ya sababu,alikwepa kodi ya Sh 173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Pia inadaiwa Kabendera alitakatisha Sh 173,247,047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na ukwepaji kodi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/37wLyab
via
logoblog

Thanks for reading KESI YA KABENDERA YAAHIRISHWA HADI FEBRUARI 10

Previous
« Prev Post